» » Nyangumi 400 wakwama kwenye ufuo wa bahari New Zealand

Nyangumi 400 wakwama kwenye ufuo wa bahari New Zealand




Mamia wajitokeza kuwaokoa nyangumi waliokwama New Zealand

Watu wa kujitolea wanasaidia katika juhudi za kuwaokoa nyangumi karibu 100 waliokwama kwenye ufuo wa bahari.
Nyangumi hao ni sehemu ya nyangumi 400 waliokwama baharini usiku wa kuamkia leo.
Takriban nyangumi 300 walifariki usiku katika ufuo wa Farewell Spit, katika kisiwa cha Kusini, katika kisa ambacho kinatajwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Mamia ya raia wa kujitolea wakisaidiana na maafisa wa uhifadhi wa wanyama na mazingira wanafanya juhudi za kusaidia kuwarejesha nyangumi hao baharini.
Wamekusanyika kwenye foleni kubwa kujaribu kuwaokoa nyangumi hao.
Wanasayansi kufikia sasa bado hawajafanikiwa kufahamu ni kwa nini nyangumi hufika kwenye ufuo wa bahari.
Lakini wakati mwingine inadhaniwa huwa inatokea kwa sababu nyangumi ni wazee sana au wanaugua, au wameumia, au wamepoteza mwelekeo hasa maeneo ambayo ufuo si laini.
Wakati mwingine, nyangumi anapokwama baharini, atawalilia wenzake ambao watafika kujaribu kumuokoa. Wengi mara nyingi nao hukwama maji yanapokupwa.

Golden Bay, New Zealand 10 Februari 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu wa kujitolea wanajaribu kuwarejesha nyangumi hao baharini

Idara ya uhifadhi baharini imesema ilipokea taarifa kwamba huenda kuna nyangumi waliokuwa wamekwama Alhamisi usiku.

Nelson, New Zealand Ijumaa, 10 Februari 2017.Haki miliki ya pichaAP
Image captionKisa cha sasa ndicho kibaya zaidi kutokea nchini humo

Hata hivyo, hawakuanzisha operesheni ya kujaribu kuokoa nyangumi hao kwa sababu ilikuwa hatari sana kujaribu kufanya operesheni hiyo gizani, gazeti la New Zealand wameripoti.

Golden Bay, New Zealand 10 Februari 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMara kwa mara nyangumi hukwama Farewell Spit

Mada zinazohusiana

Kuwa wakwanza kupata kilicho bora kutoka 4sn news tuma namba yako whatsapp 0769436440 share Read More




Mkurugenzi +255769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...