Polisi watibua shambulizi la kigaidi Ufaransa
Njama ya kufanya shambulizi nchini Ufaransa umetibuliwa huku washukiwa wanne wakikamatwa eneo la Montpellier, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani Bruno Le Roux.
Wanaume watatu na msichanawa umri wa miaka 16 walipatikana na bidhaa za kutengeneza bomu na kikosi cha kupambana na ugaidi, wakati wa uvamizi kweye nyumba moja kusini mwa mji.
Vilipuzi vya kutengezewa nyumbani sawa na vile vilivyotumiwa wakati wa shambuliki la mji wa Paris Novemba 15 vilipatikana.
Ripoti zinasema kuwa msichanna alikuwa ameandika ujumbe wa itikadi kali mtandaoni.
Tangu mwanzo wa mwaka 2015, takriban watu 230 wameuawa kwenye mashambulizi nchini Ufaransa.
Wiki iliyopita mwanajeshi mmoja alipata majeraha madogo, wakati mwanamme moja aliyekuwa na panga alipojaribu kuingia makavazi ya mjini Paris.
Mwanamume huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 29 Abdullah Hamamy, alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya
Ripoti za awali zilisema kuwa mmoja wa washukiwa wa Montpellie, huenda akawa mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Shirika moja la habari la Ufaransa lilisema kuwa watu hao wanne, walikuwa wakipinga kushambulia eneo wanakotembea watalii mjini Paris, lakini taarifa za polisi zililiambia shirika la habari la Reuters kuwa uchunguzi haujabaini hasa ni wapi walikuwa wamelenga kushambulia.
Mkurugenzi +255769436440
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment