» » Zanzibar yaanza kulipa deni la TANESCO

Zanzibar yaanza kulipa deni la TANESCO

Image captionRais Magufuli alifanya mazungumzo na rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein

Rais wa Tanzania John Maguful, leo hi amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein kwenye Ikulu mjini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na waziri wa nishati na madini Sospeter Mwijarubi Muhongo, kaimu mkurugnezi mtendaji wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi Kahitwa Bishaija na meneja mwandamizi wa fedha wa TANESCO bwana Sadock Mugendi.

Tanesco kuwakatia umeme walio na madeni TanzaniaMagufuli aagiza Tanesco kuwakatia umeme wasiolipa TanzaniaDkt Mohamed Shein achukizwa na vitisho vya Tanesco

Wakati huo huo waziri wa nishati na madini Sospeter Mwijarubi Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme, baada ya serikali ya mapinduzi Zanzibar kuanza kulipa deni inalodaiwa na TANESCO.

Prof. Muhongo alisema kuwa Zanzibar imeanza kulipa kiasi cha shilingi bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.

Aidha Prof Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO, kulipa madeni katika kipindi cha siku 5 zilizobaki kwa kuwa wasipolipa watakatiwa umeme

Image captionRais wa kisiwa cha Zanzibar Ali Mohamed Shein

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...