» » Korea Kaskazini 'yafanyia majaribio injini mpya ya kurusha roketi'

Korea Kaskazini 'yafanyia majaribio injini mpya ya kurusha roketi'

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionKiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anasemekana ametaja uzinduzi huo kama wa "kihistoria"

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, vinasema kuwa taifa hilo limefanyia majaribio injini moja kubwa maalum yenye uwezo wa kurusha angani mtambo wa Satellite.

Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, amenukuliwa akisema kuwa, injini hiyo mpya itaisaidia Korea Kaskazini, kufikia uwezo wa kimataifa wa kufyatuaji Satellite angani.

Wachanganuzi wanasema majaribio ya mtambo huo wa kurusha angani roketi--ambayo bado haijathibitishwa-- pia itakuwa jambo la kuangaliwa kwa undani katika nia ya Pyongyang kuunda zana za kinuklia zenye masafa marefu.

China yaionya Marekani kuwa makini na Korea KaskaziniJe dunia itaifanya nini Korea Kaskazini?China: Marekani itatue mgogoro wake na Korea KaskaziniMwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini

Tangazo hilo linatokea wakati wa waziri wa maswala ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, anapofanya mazungumzo na viongozi wa China huko, Beijing.

Awali, Bwana Tillerson, aliionya Marekani kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, kwamba inaweza kuharibu mambo hata zaidi.

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...