» » Dereva azua hofu ya bomu ikulu ya White House

Dereva azua hofu ya bomu ikulu ya White House

Haki miliki ya pichaAFP/GETTYImage captionKikosi cha kumlinda rais kikipiga doria ikulu

Mtu mmoja anazuiwa na polisi baada ya kuendesha gari hadi kwenye kuzuizi cha ikulu cha Marekani Jumamosi usiku, kwa mujibu wa kikosi cha kumlinda rais.

Ulinzi kwenye ikulu ya White House uliongezwa mara moja. Kituo cha CNN kinasema kuwa dereva wa gari hilo alidai kuwa na bomu.

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa jimbo la Florida wakati kisa hicho kilitokea.

Kikosi kinachoilinda ikulu ya White House kinasema kuwa dereva alikaribia kizuizi cha ikulu mwendo wa saa 03:05 GMT.

Trump aondoshwa jukwaani na maafisa wa usalamaMcMaster awa mteule mpya wa Rais TrumpMwanajeshi aikataa kazi ya Trump

Kisha dereva wa gari hilo alikamatwa.

Kisa hicho ndicho cha pili kutokea White House, baada ya mtu mmoja mapema kuruka eneo la kuegeshwa baiskeli kwenye ua unaouzunguka White House.

Kikosi cha kumlinda rais kimekosolewa vikali wiki hii baada ya kisa cha mtu mmoja kuruka ua tarehe 10 mwezi Machi na kuikaribia ikulu.

Jonathan Tran mwenye umri 26, alikaa ndani ya uwanja wa White House kwa zaidi ya dakika 16 kabla ya kukamatwa.

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...