Washambuliaji wa kujitoa mhanga wawaua watu Nigeria
Image captionNigeria
Washambuliaji wa kujitolea mhanga kaskazini mwa Nigeria, wameuwa watu wane, wakiwemo mwanamke na watoto wake wawili.
Watu kama wanane walijeruhiwa katika kijiji, karibu na mji wa Maiduguri.
Msemaji wa polisi, Viktor Isuku alieleza kuwa washambuliaji watatu mwanamume na wanawake watatu, walijilipua kwa mabomu, walipokabiliwa na kundi la wanamgambo watiifu kwa serikali.
Wasichana 2 washambuliaji wa kujitolea mhanga wauawa NigeriaMsichana wa miaka 10 ajilipua Nigeria
Mwanamgambo mmoja pia alikufa katika shambulio hilo.
Maiduguri ndiko lilipoanza kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, ambalo limeuwa watu elfu 15, tangu lilipoanza kupigana dhidi ya serikali ya Nigeria, miaka minane iliyopita.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionBoko Haram, limewaua watu elfu 15, tangu lilipoanza kupigana dhidi ya serikali ya Nigeria, miaka minane iliyopita.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment