Winnie Mandela alazwa hospitalini Johannesburg.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionWinnie Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela
Shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela, amelazwa hospitalii kwa kile kinachotajwa kuwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Familia yake inasema kuwa alipelekwa hospitali ya Milpark mjini Johannesburg.
Mwezi Disemba mwaka uliopita, Bi Madikizela-Mandela alilazwa hospitali hiyo lakini kile kilichosababisha alazwe hakikutajwa.
Winnie Mandela aukosoa uongozi wa ANCWinnie Mandela aibiwa dola 6000 kutoka nyumbani kwakeRaia wa Malawi na DRC miongoni mwa wanawake 100 wa BBC
Msemaji wake Victor Dlamini, aliambia BBC kuwa alikuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida lakini madaktari wakaamua kumlaza.
Bi Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela, na alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kusajiliwa kama mhudumu wa kijamii nchini Afrika Kusini.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment