» » Mahakama yazuia kuuawa kwa wafungwa Arkansas, Marekani

Mahakama yazuia kuuawa kwa wafungwa Arkansas, Marekani


Don Davis na Bruce WardHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMahakama imezuia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya Don Davis na Bruce Ward
Mahakama ya Juu katika jimbo la Arkansas nchini Marekani imetoa agizo la kuzuia kuuawa kwa wafungwa wawili kati ya wanane ambao wamepangiwa kuuawa kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Mawakili wa wafungwa hao, ambao walipatikana na makosa ya mauaji, wameibua maswali kuhusu hali ya kiakili ya wafungwa hao.
Serikali ya Arkansas imesema itakata rufaa uepesi kupinga uamuzi huo.
Katika uamuzi mwingine, mahakama hiyo pia iliondoa agizo la muda la kuzuia kuuawa kwa wafungwa hao wanane.
Jimbo la Arkansas linataka kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wafungwa hao haraka iwezekanavyo kwa sababu shehena yake ya dawa za kutumiwa kuua wafungwa inakaribia kufikisha muda wake wa mwisho kutumika.
Dawa hiyo aina ya Midazolam itafikisha muda wake wa mwisho wa kutumika mwishoni mwa mwezi Aprili.
Mahakama ilikuwa imetoa agizo la muda Jumamosi kwamba wafungwa hao hawangeuawa kwa sababu shindano hiyo ya sumu ingewasababishia dhiki.
Watetezi wa haki wamepinga kutumiwa kwa dawa hiyo.
Wanaume hawa walifanya nini?
Don Davis, Stacey Johnson, Jack Jones and Ledell Lee; left to right, bottom: Jason McGehee, Bruce Ward, Kenneth Williams na Marcel WilliamsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanane hawa walipangiwa kuuawa kabla ya Jason McGehee (wa kwanza kushoto) akaondolewa kwenye orodha hiyo
Bruce Ward - Alimnyonga kijana mhudumu wa duka Rebecca Doss
Don Davis - Alimuua ane Daniel alipokuwa akitekeleza wizi
Stacey Johnson - Alimuua Carol Heath, ambaye alichapwa na kunyongwa kisha kukatwa shingo
Ledell Lee - Alimuua Debra Reese kwa kumpiga kwa kipande cha chuma
Jack Jones - Alimbaka na kumuua Mary Phillips
Marcel Williams - Alimbaka na kumuua Stacey Erickson, baada ya kumteka kutoka kwenye duka moja
Kenneth Williams - Alimuua mkulima Cecil Boren wakitoroka gerezani ambapo Williams alikuwa amefungwa kwa kumuua Dominique Hurd
Mbona suitafahamu?
Sawa na majimbo mengine mengi Marekani, jimbo la Arkansas limetatizika kupata dawa za kutumiwa kuwaua wafungwa.
Mara ya mwisho wafungwa kuuawa jimboni humo ilikuwa mwaka 2005.
Maswali kuhusu Midazolam yalianza kuulizwa baada ya wafungwa katika majimbo matatu Marekani kuchukua muda mrefu kuliko kawaida walipokuwa wakiuawa mwaka 2014.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...