Watu kadha wapigwa
risasi kwenye klabu nchini Marekani
·
dha wapigwa risasi kwenye klabu nchini Marekani
Mtu mmoja ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa kufuatia ufyatuaji wa
risasi kwenye klabu ya usiku huko Cincinati jimbo la Ohio.
Takriban watu wawili waliokuwa na silaha walitekeleza shambulizi
kwa mujibu wa polisi.
Watu kadha walipata majeraha mabaya.
"Tuko kati kati ya hali mbaya alisema mkuu wa polisi"
Paul Neudigate.
Kapteni wa polisi Kimberly Williams alisema kuwa polisi hawana
taraifa kuhusu washambuliaji hao.
Hadi wakati huu kile kilochosababisha kutokea ufyatuaji huo bado
hakijulikani.
Ufyatuaji huo ulitokea saa 05:00 GMT wakati mamia ya wtu
walikuwa eneo hilo.
Kisa hicho kinatokea chini ya mwaka baada ya Omar Mateen,
kufyatua risasi kwenye klabu ya wapenzi wa jinsia moja mjini Orlando huko
Florida.
Mateen aliwaua watu 49 katika kisa ya kibaya zaidi cha ufyatuaji
risasi katika historia ya Marekani.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment