» » Maonesho ya kijeshi yafanyika Urus

Haki miliki ya pichaAFPImage captionBw Putin (kushoto) alivalia kitambaa cha rangi nyeusi na dhahabu kwenye koti - ishara ya uzalendo

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesifu kujitolea mhanga na kujitoa kafara kwa watu wa Muungano wa Usovieti wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Bw Putin alisema hayo wakati wa maonesho ya kila mwaka ya majeshi ya taifa hilo kuadhimisha Siku ya Ushindi ambayo hutumiwa kukumbuka ushindi katika vita hivyo.

Kwa mara ya kwanza, maonesho hayo ya kijeshi yalishirikisha makombora ambayo yameundwa mahsusi kwa vita katika maeneo yenye baridi kali ya Arctic.

Urusi inajenga kambi mpya za kijeshi Arctic.

"Hakuna nguvu zozote zitakazoweza kuwashinda watu wetu," Bw Putin alisema, na kulaani uharibifu na maafa yaliyosababishwa na Ujerumani wakati wa vita hivyo.

Muungano wa Usovieti ulipoteza zaidi ya watu 20 milioni, zaidi kuliko taifa lolote lile wakati wa vita hivyo.

Muungano wa Usovieti (USSR) ulivunjika mwaka 1991.

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionWanajeshi wa urusi wakati wa maonesho tarehe 9 Mei 2017

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko naye alishiriki katika sherehe ya kuweka shada la maua katika makumbusho mjini Kiev.

Aliwaambia wanajeshi wa Ukraine kwamba Urusi inajaribu kutumia maadhimisho ya ushindi huo "kutimiza mahitaji yake ya kikoloni na upanuzi."

"Kremlin bado inajaribu kuiamrisha Ukraine kama ilivyofanya ilipodhibiti maeneo manne ya vita Ukraine miaka ya 1940."

Urusi imekuwa ikishutumiwa na kudaiwa kudunisha mchango wa nchi nyingine katika vita vya kushinda utawala wa Nazi nchini Ujerumani.

Mataifa ya Magharibi yaliiwekea vikwazo Urusi baada yake kutwaa udhibiti wa eneo la Crimea mwaka 2014.

Urusi pia imekuwa ikituhumiwa kuunga mkono wapiganaji wanaopigania kujitenga kwa maeneo ya mashariki mwa Ukraine.

Vita Vikuu vya Dunia vinakaribia?China 'yaeleza wasiwasi' kuhusu Korea Kaskazini

Urusi imekanusha tuhuma kwamba inasaidia waasi hao kijeshi, lakini imekiri kwamba Warusi wa "kujitolea" wanasaidia waasi.

Jeshi la vijana

Miongoni mwa zana za kivita ambazo zilioneshwa Red Square Jumanne, kulikuwa na makombora ya Pantsir-SA ya kujilinda sana ya kutumiwa maeneo ya Arctic.

Kulikuwa na makombora ya Yars RS-24 ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine. Makombora hayo yanaweza kutumiwa kurusha silaha za nyuklia.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMakombora ya nyuklia ya Yars RS-24: Maonyesho hayo yamefufua kumbukumbu za maonyesho ya kijeshi ya Muungano wa Usovieti enzi za Vita Baridi

Wanachama wa jeshi mpya la "vijana wazalendo" ambalo linaitwa Yunarmiya, pia walishiriki maonesho hayo kwa mara ya kwanza.

Hafla kuu ilifanyika Moscow, lakini maonesho mengine yalifanyika katika miji mbalimbali Urusi. Miji mingi iliyoandaa maonesho ni ile iliyoathiriwa sana na vita hivyo vya 1941-1945 ambavyo Urusi huviita "Vita Vikuu vya Kizalendo".

Haki miliki ya pichaAFPImage captionWanajeshi wa majini wa Urusi: Jeshi la Urusi limekuwa likijisifia kutokana na uwezo wake wa kupigana vita maeneo ya Arctic

"Ili kuushinda ugaidi, na misimamo mikali na itikadi mpya za Nazi, tunahitaji ushirikiano wa jamii yote duniani," Bw Putin alisema kwenye hotuba fupi.

Uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini

Urusi imekuwa ikitumia silaha zake mpya katika vita vya Syria, ambapo wanajeshi wa nchi hiyo wanasaidia wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar al-Assad.

Wanajeshi wa Assad pia husaidiwa pakubwa na Iran.

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionWanajeshi wa miavuli wa Urusi wakati wa maoneshoHaki miliki ya pichaAFPImage captionMakombora ya kujilinda ya Pantsir-SA yakiwa na kamafleji ya rangi nyeupe mahsusi kwa vita ArcticHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionMizinga ikifyatuliwa nje ya ukuta wa KremlinHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionWanajeshi wa kike: Wanajeshi wengi wa kike walipigana dhidi ya NaziHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionVifaru vikiwa Red Square wakati wa maonesho

Mada zinazohusiana

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...