Sehemu ya 1, HISTORIA NA CHIMBUKO LA BABELI
Ili tuweze kuelewa BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCH, ni nani, ni muhimu tukaijua historia ya BABELI kwanza, ujuzi huo utauongoza KUMFAHAMU HUYO BABELI MKUU.
Kihistoria Babeli ilianza zamani sana, zamani kabla hata ya kuwapo kwa taifa la Israeli. Tukirejea katka maandiko kwenye Mwanzo 11, tunaliona Chimbuko la Babeli.
Hapo katika Mwanzo 11, tunagundua kuwa Babeli ilitokana na "UASI DHIDI YA MUNGU" Watu hawa waliamua kwa makusudi kabisa "KUKIUKA MAAGIZO YA MUNGU NA KUJENGA MNARA DHIDI YA MUNGU!"
Mungu hakuweza kuuvumilia ukaidi huo uliopitiliza, hivyo akaamua kuingilia kati na kusimama dhidi ya mpango wao, kwa kuichafua lugha, mpango wao ukakwama.
Hivyo basi, zingatia kuwa BABELI ILITOKANA NA MGOGORO, AU USHINDANI DHIDI YA MUNGU. Babeli ni zao la uasi dhidi ya Mungu na utaratibu wake, ni zao la VITA DHIDI YA MUNGU.
Ni muhimu sana upaelewe hapa, ili uweze kuelewa vyema huko mbele.
Wakati huo Babeli ilikuwa chini ya utawala wa mtawala aliyekuwa akiitwa NIMRODI. Mtawala ambaye kwa macho ya Wababeli alikuwa ni mtawala aliyetukuka sana. Baada ya kifo chake huyo NIMRODI iliaminika AMEBADILIKA NA KUWA MUNGU JUA.
Wababeli walianza kumuabudu na kumtukuza kama MUNGU MKUU, MUNGU JUA.
Ibada hii ya kumuabudu mungu jua ilienea na kutawala karibu dunia nzima kwa karne nyingi sana,
Wamisri ambao ndio waliokuja kuwa watawala wa dunia baada ya Babeli kuanguka walimuabudu mungu jua huyo pia, kwao alikuwa akiitwa "mungu Ra".
Hata Babeli ya baadae ya Nebukadreza, pia walipiga goti kumuabudu huyo mungu jua Nimrod, kwao alikuwa akifahamika kama "mungu beli (beli maana yake ni jua, kikaldayo)" na pia ushahidi wa kihistoria unaonyesha hata waajemi, waliokuja kuitawala dunia baada ya Babeli walimuabudu pia mungu jua.
Ibada hiyo ya mungu jua ilikuwa na ushawishi mkubwa sana duniani, kiasi kwamba HATA WATU WA MUNGU ISRAELI, WALIOKUWA WAKIMJUA MUNGU WA KWELI MUUMBAJI, HAWAKUSALIMIKA NA IBADA HIYO, WALIJIKUTA WANAPIGA GOTI KUMUABUDU MUNGU JUA.
>"Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki".
EZEKIELI 8 : 16.
Hapo unaona kabisa watu hao wa Mungu Muumbaji, walijikuta wanapiga magoti kumuabudu mungu jua tena wakiwa ndani ya Hekalu Takatifu la Mungu Muumbaji.
Si hivyo tu, bali pia katika zama za mfalme Ahabu kipindi Eliya akiwa nabii katka Israeli, ibada kwa mungu jua ilikuwa imeliteka karibu taifa lote kabisa la Mungu Muumbaji. Eliya alifanya kazi kubwa sana kuwarejesha watu katika ibada kwa YEHOVA. Maana taifa zima la watu wa YEHOVA walikuwa wamezama kabsa kabisa katka kumuabudu Baali (BAALI NI MUNGU JUA).
Tumeona kuwa ibada hii ya kipagani ya mungu jua ilivyowateka hata watu wa Mungu zama hizo,
Je, sisi watu wa Mungu wa leo hatujatekwa na ibada hiyo potofu ya kumuabudu mungu jua?
Tutatazama hilo katka masomo yajayo katika mfululizo huu.
TAMUZI
Semiramis alikuwa mke wa Nimrod enzi za uhai wake. Lakini baada ya Nimrod kufa, mama huyo alipata ujauzito, ndipo ikaaminika kuwa amepewa ujauzito huo na marehemu mumewe mabaye kwa wakati huo si mtu tu, bali ni mungu jua. Hivyo ikaaminika kuwa mimba hiyo ni ya mungu jua.
Mtoto alipozaliwa alipewa heshima ya "mwana wa mungu" maana alitokana na mungu jua, kwa mujibu wa imani yao. Mtoto huyo alizaliwa usiku wa tare 24 Dec, kuamkia tarehe 25 Dec, na alikuwa akiitwa TAMUZI. Hata hivyo hakuishi sana, alikufa mapema tu.
Tangu wakati huo aliheshimika pote duniani kama "mungu mwana", mwana wa mungu mkuu, mungu jua! kote ambako ibada ya mungu jua ilifika, pia walikuwa wakimuabudu huyo TAMUZI wakimtambua kama "mungu mwana".
Hata katika Israeli kwa watu wamjuao Mungu wa kweli, hawakusalimika na ibada hii ya kumuabudu TAMUZI.
Biblia inaonyesha wazi
"Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya BWANA, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi".
EZEKIELI 8 : 14
Kama ilivyokuwa kwa mungu jua, vivyo hivyo Waisraeli waliipokea ibada ya Tamuzi na kuiingiza hekaluni mwa BWANA, kuiingiza hekaluni maana yake, ni kuichanganya na ibada kwa YEHOVA.
Hivyo Waisraeli wakawa wanakwenda hekaluni kumuabudu Yehova, lkn ndani ya ibada hiyo hiyo ya Yehova wakawa wanaichanganya na ibada kwa mungu jua, na kwa mungu Tamuzi.
Hiyo ni mbinu mama ya Babeli katika kuwapotosha watu wa Mungu.
SEMIRAMIS
Semiramis baada ya kumzaa TAMUZI, nae pia akapewa heshima ya kuitwa "mama wa mungu" maana, ndo aliyemzaa mungu Tamuzi. Alijulikana pia kama "mungu mama" na jina lake maarufu jingine, Alijulikana kama "MALKIA WA MBINGUNI"
Huyu pia aliabudiwa kote ambako mungu jua aliabudiwa.
Hata katika Israeli watu wa Mungu pia walijikuta wanamuabudu huyo MALKIA WA MBINGUNI.
> " Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.
YEREMIA 7 : 18,
Soma pia Yeremia 44: 17, Yeremia 44 : 18 nk.
*****************
Hivyo Babeli zamani sana miaka elfu kadhaa kabla ya BWANA NA MWOKOZI WETU KUZALIWA HAPA DUNIANI,
Tayari walikuwa wakimuabudu mungu aliyekuwa na siku yake maalum jumapili.
Walikuwa wakimuabudu mungu mwana Tamuzi, ambaye sherehe yake kubwa ilikuwa ikifanyika Dec 25, birthday yake.
Na pia walikuwa wakimuabudu semiramis mama wa Tamuzi, ambaye alikuwa akitambulika kama mama wa mungu, mungu mama, na malkia wa Mbinguni, hii ni karne nyingi kabla ya uwepo wa Bikira Mariamu.
Ibada hiz, ndio msingi wa upotoshaji wa BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI!
Upotoshaji huo uliandaliwa mapema sana kwa lengo la kuja kupinga na kuipotosha huduma ya Yesu duniani.
Kwa leo tunakomea hapo, endelea kufuatilia mfululizo huu, kwa ufafanuzi zaidi wa siri za Babeli
No comments:
Post a Comment