Polisi 40 wauawa kwa
kukatakatwa Kasai, DR Congo
·
Wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
wamewashambulia na kuwaua kwa kuwakatakata wanajeshi takriban 40 baada ya
kuwavizia katika mkoa wa Kasai, katikati mwa nchi hiyo, maafisa wa serikali
wamesema.
Wapiganaji hao kutoka kundi la Kamwina Nsapu walishambulia
polisi waliokuwa kwenye msafara.
Maafisa sita wa pilisi waliowasiliana na Tshiluba waliachiliwa
huru, rais wa bunge la jimbo la Kasai Francois Kalamba amesema.
Machafuko jimbo la Kasai yalianza Agosti mwaka jana, pale
maafisa wa polisi walipomuua kiongozi wa Kamwina Nsapu.
Shambulio la Ijumaa lililenga msafara wa polisi waliokuiwa
wakisafiri kati ya Tshikapa na Kananga.
Gavana wa jimbo hilo Alexis Nkande Myopompa amesema uchunguzi
umeanzishwa kuhusu mauaji hayo.
Umoja wa Mataifa unasema watu 400 wameuawa na wengine 200,000
kuachwa bila makao eneo la Kasai tangu Jean-Pierre Pandi, kiongozi wa Kamwina
Nsapu alipouawa.
Mauaji yake yalitekelezwa miezi miwili baada ya Kamwina Nsapu
mwezi Juni 2016 kuanzisha juhudi za kutaka atambuliwe kama mkuu wa eneo hilo na
kutaka maafisa wa serikali ya taifa kuondoka jimbo hilo.
Umoja wa Mataifa unasema umepata makaburi 10 ya pamoja ambapo
waliouawa katika machafuko hayo walizikwa.
Kadhalika, kuna maeneo mengine saba ambapo inadhaniwa kuna
makaburi yaliyozikwa watu wengi kwa pamoja.
Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa, Mmarekani na raia wa
Sweden, walitekwa nyara eneo hilo wiki mbili zilizopita pamoja na raia wanne wa
DR Congo waliokuwa wakifanya kazi nao.
Kufikia sasa bado hawajulikani walipo.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMaafisa wa usalama DR Congo wamekuwa wakikabiliana na waasi maeneo
mbalimbali nchini humo
DR Congo imekabiliwa na hali ya wasiwasi kisiasa huku Rais
Joseph Kabila akiendelea kukaa madarakani kwa muda zaidi kuliko alivyoruhusiwa
kikatiba.
Muhula wake ulimalizika Desemba mwaka jana.
Uchaguzi umepangiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu
lakini tarehe kamili haijaafikiwa.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment