» » Usomaji wa biblia kwa mpango na ufafanuzi

Biblia: Soma, Elewa, Shuhudia"

USOMAJI WA BIBLIA  KWA MPANGO*
http://tgvs.org/archives/2301
(a) *19-125:* Zaburi 125
(b) *Kategoria:* Zaburi
(c) *Mfululizo:* Biblia Sura kwa Sura
(d) *Wahusika:* Bwana, watu Wake
(e) *Tabia ya Mungu:* Uaminifu, Umilele
(f) *Fungu Kuu:* Zaburi 125:1
(g) *Neno Kuu:* Ulinzi, Zaburi 125:2
(h) *Msisitizo:* Mtumainie Bwana
_________________________

*MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU*
(1)Kumtumainia Bwana
(2)Wakaa milele.
(3)Bwana huzunguka watu Wake
(4)Tangu sasa na hata milele.
(5)Fimbo ya udhalimu
(6)Bwana ni mwema
(7)Walio wanyofu wa moyo.
(8)Watenda maovu
(9)Amani ikae na Israeli
___________________________

ZABURI 125

1 *Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni,* Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, *Tangu sasa na hata milele.*

3 Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.

4 Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo.

5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
__________________________

*MASWALI MUHIMU KATIKA SURA HII*

(1) Je, mada kuu ni nini hapa?
(2) Je, wahusika wakuu ni nani hapa?
(3) Je, fundisho kuu ni lipi hapa?
(4) Je, kuna dhambi ya kuepuka hapa?
(5) Je, kuna dhambi ya kutubu hapa?
(6) Je, kuna ombi la kuomba au kurudiwa hapa?
(7) Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
(8) Je, kuna agizo au wajibu wa kufanya hapa?
(9) Je, kuna makosa au mapungufu ya kuepukwa hapa?
(10) Je, sura hii inafundisha mimi nini kuhusu Mungu?
(11) Je, sura hii ina umuhimu gani kuhusu mpango wa wokovu wangu?
_________________________

*TUFANYE NINI BASI NA SURA HII?*
(1)Jambo la kukumbukwa tena na tena
(2)Ombi, Shukrani na Sifa kwa Mungu
(3)Tufanye Nini Basi?
_______________________

*SAUTI YA INJILI*
Sikiliza Sauti ya Mungu kwako leo tunapofunga kipindi hiki

📖 Isaya 54:10

Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; *bali wema Wangu hautaondoka kwako, wala agano Langu la amani halitaondolewa;*  asema Bwana akurehemuye. 🙏🏼
__________________________

*MWITIKIO WETU*

NZK # : 128. Taamini Nitii Pia
_(When We Walk with the Lord)_

1.🎼 🎼
Namwandama Bwana kwa alilonena,
Njia zangu huning'azia;
Na nikimridhisha, atanirudisha,
*Taamini nitii pia.*

▪Kuamini, Njia pweke ni hii
▪Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.

2.🎼 🎼
Giza sina kwangu wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi;
*Huamini nitii pia.*

3.🎼 🎼
Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki.
*Taanimi nitii pia.*

4.🎼 🎼
Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili,
*Taamani nitii pia*

5.🎼 🎼
Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
*Huamini, nitii pia.*
__________________________

*NITAPATAJE SOMO LA LEO?*

Pakua Mobile App: The Gospel’s Voice
*Facebook:* Sauti Ya Injili SDA
*Whats App:* Sauti Ya Injili SDA

*WAWEZA PIA KUSIKILIZA KUPITIA:*
▪Kiungo cha TGV Mobile App
▪Kiungo cha Tovuti: Sauti Ya Injili SDA
_________________________

*BWANA ATUBARIKI SOTE!*

The Gospel’s Voice © 2017

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...