» » Korea Kusini imewaongezea fedha wale wanaokimbia Korea Kaskazini hadi dola 860,000

Korea Kusini imewaongezea fedha wale wanaokimbia Korea Kaskazini hadi dola 860,000

Haki miliki ya pichaAPImage captionMpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini ni moja ya maeneo yenye ulinzi wa juu zaidi duniani

Korea kusini imeidhinisha nyongeza ya fedha inazotoa kama malipo kwa watu wanaoasi uraia wao kutoka nchi jirani ya Korea Kaskazini,kwa lengo la kupata habari muhimu za kujasusi.

Hatua hiyo pia ina walenga wanajeshi wanaovuka mpaka wakiwa na zana za kijeshi.

Waasi waliyo na taarifa muhimu itakayo saidia kuimarisha usalama wa Korea Kusini, watapokea,fedha ya hadi dola 860,000

Wizara ya masuala ya muungano imesema, sheria hiyo mpya, itaongeza ruzuku ya vifaa vitakavyo ingizwa nchini humo na waasi hao.

Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia atimuliwaPolisi nchini Malaysia wagundua kilichomuua Kim Jong NamMshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90

Vifaa hivyo ni kama vile meli na karakana ya kijeshi.

Hii ni mara ya kwanza kwa nyongeza kama hiyo kutolewa katika kipindi cha miaka ishirini.

Lengo la hatua hiyo ni wazi kuwa, Korea Kusini inataka kuongeza idadi ya watu wanaobadilisha uraia wa Korea kaskazini kujiunga nayo.

Serikali ya Korea Kaskazini bado haijatoa tamko lolote juu ya hatua hiyo ya Korea Kusini.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...