» » Wajiua Huku Wakijirekodi Facebook


facebook
Jay Bowdy (Kushoto) na  Nakia Venant (Kulia).
MWANAUME mmoja nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Jay Bowdy, 34, ambaye pia ni muigizaji chipukizi amekutwa akiwa amejiua garini huku taarifa zikisema kwamba kabla ya kujiua, aliwaambia wafuasi wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook kwamba anajiua hivyo wawapigie simu polisi kutoka hapo Los Angeles na kuwaambia kwamba alikuwa akijiua.
Baada ya kupewa taarifa na raia wema, polisi kutoka katika kituo kikuu hapo Los Angeles walijaribu kumpigia jamaa aliyelipaki gari lake katika ya Mitaa ya Cumpston na Fulcher lakini hawakuweza kumpata kwa kuwa tayari alikuwa amekwishatekeleza kile alichokitaka.
Watu waliokuwa wakifuatilia tukio hilo katika video hiyo iliyokuwa ikirekodiwa ‘live’ walipigwa na bumbuwazi kwani wengi walihisi kwamba alikuwa akiigiza kutokana na kazi yake hiyo kumbe mshikaji alikuwa akijiua kweli. Baadaye video hiyo ikatolewa mtandaoni na Facebook.
SABABU YA KUJIUA
Chanzo kilichokuwa hapohapo Los Angeles kinasema kwamba inawezekana Jay mwenye watoto wanne alijiua baada ya kupata msongo wa mawazo kwani alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumdhalilisha kijinsia mwanamke mmoja huku akitakiwa kumlipa kiasi cha dola laki moja ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200.
MWINGINE NAYE AJIUA
Huku zikiwa hazijapita hata saa 12, msichana mmoja, Nakia Venant ‘14’ anayeishi Jijini Miami alifanya kama alivyofanya Jay kwa kujirekodi akiwa bafuni na kisha kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia taulo lake alilolifunga bafuni mapema wiki hii.
Kifo cha Nakia kimezua hofu kwa wazazi wa maeneo hayo na polisi wa Jimbo la Florida wamesema kwamba wanaendelea kuchunguza kifo cha msichana huyo ambacho kimeonekana kuwa cha kipekee kwa kitendo cha kujirekodi ili wafuasi wake watazame anavyokufa.⠀
Mtu aliyeona tukio hilo na kumtambua mhusika alikuwa rafiki wa msichana huyo ambapo mara moja akawataarifu polisi na kuwaeleza kilichokuwa kikiendelea ambapo mpaka polisi wanafika eneo la tukio, tayari Nakia alikuwa amekwishafariki dunia.
Polisi hao wamewaambia waandishi wa habari kwamba kilichowafanya kuchelewa kufika huko ni kwamba rafiki wa Nakia alikosea kuwapa anwani ya kufika huko, kitu kilichowafanya kupotea, mpaka wanapata anwani yenyewe, wakawa wamekwishachelewa kufika huko kwa wakati.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...