KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI-MARCH 05,2017
*somo* KUUNGANIKA TENA
_"Tena iweni wafadhili ninyi Kwa ninyi, wenye huruma,mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi_ *"Waefeso 4 : 32.*
____________
Wakati Yakobo akipambana na Malaika, mjumbe mwingine wa mbinguni alitumwa Kwa Esau.ndotoni, Esau alimwona nduguye akiwa uhamishoni toka nyumbani
kwa baba yake kwa miaka
Ishirini ;alimwona akiwa amezingirwa na majeshi ya Mungu.
Esau aliisimulia ndoto hii kwa askari wake, huku akiwagiza wasimdhuru Yakobo, kwani Mungu wa baba yake alikua pamoja naye.
Hatimaye ,haya makundi mawili yalikaribiana,kiongozi wa jangwa akiongoza watu watu wake wa vita na Yakobo pamoja na wakeze na watoto ,huku wakiwa wamefuatana na wachungaji wa kondoo na wasaidizi wakifuatiwa na
mistari mirefu ya mifugo na wanyama.
huku akitegemea fimbo yake ,mzee huyu wa imani alitangulia kukutana na kundi hili la askari.alikua amepauka na mlemavu kutokana na pambano lake la hivi karibuni na alitetembea taratibu kwa maumivu, akisimama katika kila hatua; lakini uso wake ulingazwa kwa amani.
Mara alipomwona huyu mlemavu alieteseka, "Esau alikuja akaja mbio kumlaki,akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia."walipoangalia tukio hili, hata mioyo ya askari wakatili wa Esau iliguswa. Licha ya ndoto ambayo alikua ameambiwa, hawakuweza kuelewa badiliko ambalo lilikua limetokea kwa kiongozi wao.
Japo walikua wameona udhaifu wa mzee huyu wa imani, hawakufikiri kwamba huu udhaifu wake ulikuwa umefanywa kuwa nguvu yake.
Katika usiku wake wa taabu pale kando ya Yaboki, wakati uangamivu ulipoonekana kuwa mbele yake, *Yakobo akafundishwa jinsi msaada wa binadamu usivyofaa chochote, jinsi tegemeo katika nguvu ya binadamu lisivyo na msingi wowote. Aliona kwamba ilikua ni lazima msaada wake wa pekee utoke Kwake yeye ambaye alikua amemkosea vibaya kiasi kile.Huku akiwa hajiwezi na asiyestahili ,alisihi ahadi ya Mungu ya rehema itimizwe kwa mwenye dhambi anaetubu.*
Ahadi hio ilikuwa ndio uhakika Kwake kwamba Mungu angemsamehe na kumkubali.
Hata kama mbingu na nchi zingepita
ahadi hio isingepita;na ilikua ni hii ambayo ilimshikilia katika kipindi
hiki cha pambano la kutisha.
----------
Rehema za Bwana ni MPYA KILA SIKU Asubuhi *maombolezo 3:22-23*
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
tupe maoni yako
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment