UN yalaani mauaji ya
watoa misaada Sudan Kusini
Umoja wa mataifa umelaani vikali mauaji ya wafanyakazi sita wa
kutoa misaada nchini Sudan Kusini.
Miongoni mwa waliouawa ni raia watatu kutoka Kenya, na watatu
kutoka Sudan Kusini ambao walitekwa siku ya Jumamosi walipokuwa wakisafiri
kutoka mji mkuu Juba kwenda mji wa Pibor.
Hili ni tukio la tatu la aina hiyo ndani ya mwezi mmoja likiwa
limepoteza maisha ya watu wengi tokea kuanza kwa mgogoro huo mwaka 2013.
Mkuu wa mashirika ya kibinaadam nchini Sudan Kusini Eugene Owusu
ameelezea mauaji hayo kama uhalifu wa kutisha.
Wafanyakazi 12 wa mashirika ya kutoa misaada waneuawa mwaka huu,
wakati huu ambapo wanajaribu kuelekea sehemu ambazo umaskini ni mkubwa kutokana
na vita.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment