Rais Magufuli amfuta
kazi katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli
amemfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Prof. Justin Ntalikwa.
Rais Magufuli amefanya hivyo siku chache baada ya kufanya ziara
ya kushtukiza bandarini. Hata hivyo, haijabainika iwapo kuna uhusiano kati ya
ziara hiyo na kufutwa kwake Ntalikwa.
Rais Magufuli alifanya ziara hiyo kwa lengo la kufuatilia
utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti, juu ya kudhibiti
udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo, ikiwemo
usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli alishuhudia makontena 20 ya
mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa, ambayo
yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku
usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 2 Machi, 2017.
Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Rais Magufuli alimuagiza
mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP - Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola,
kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi
wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.
Akiwa bandarini hapo Rais Magufuli pia, alishuhudia udanganyifu
mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje, ya nchi
baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonyesha yamebeba mitumba ya
nguo na viatu, wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya
kifahari.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment