Uber yaondoa magari
yanayojiendesha barabarani baada ya ajali
Kampuni ya Uber imeondoa magari yake yanayojiendesha barabarani,
baada ya ajali ambapo moja ya magari yake lilianguka.
Picha zilizochapishwa zilionyesha gari lilokuwa limepinduka
kwenye barabara katika jimbo la Arizona, kando na gari lingine lililokuw
limeharibika vibaya.
Gari hilo aina ya Volvo SUV lilikuwa likijiendesha lenyewe
wakati wa ajali. Hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Msemaji wa polisi eneo la Tembe huko Arizona, alisema kuwa
ajalia hiyo ilitokea wakati gari lingine la Uber lilishindwa kugeuka upande wa
kushoto.
Magari ya Uber yanayojiendesha kala mara huwa na mtu kwenye kiti
cha dereva ambaye anaweza kuchukua usukani.
Kisa hicho kinajiri majuma kadha baada ya kampuni hiyo ya texi,
kukumbwa na taarifa zisizo za kuridhisha zinazohusu mazingira ya kufanya kazi.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment