Lewis Hamilton ana
imani ya kumshinda Sebastian Vettel
Dereva wa magari ya Langalanga Muingereza Lewis Hamilton anasema
ana uhakika atamshinda Sebastian Vettel katika mashindano ya dunia ya
Australian Grand Prix.
Hamilton alimaliza wa pili kwa Mjerumani huyo wakati wa kuanza
kwa msimu mjini Melbourne, kufuatia shinikizo la mwendo wa kasi wa dereva huyo
wa Ferrari.
Haki miliki ya pichaAPImage captionVettel akiongoza
"Litakuwa shindano kali, nina imani kuwa
tutawashinda," Hamilton alisema .
"Ni vizuri tutakuwa shindano hili kali"
"Kuna kazi kubwa mbeleni, tuna mengi ya kufanya lakini hata
hivyo tuko na furaha," alisema Vettel.
Hamilton naye amesema kuwa anachotarajia ni ushindani ulio mkali
na Vettel mwaka huu wote.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment