Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha
Kwa vile kijana anaisukuma
baiskeli hiyo na mikono yake miwili, hana njia ya kuwafukuza nzi kutoka kwa
macho yake.
Jina lake ni
"Mulangani". Jina hilo ni la jamii ya Nguni linalomaanisha
"niadhibu" au yule ambaye ni lazima adhibiwe. Chris Haslam alimuuliza
dereva kuhusu ni nani anayeweza kumpa mtota wake jina baya kama hilo?
"Labda babu yake au chifu," dereva akajibu.
Nchini Zambia na hata Zimbabwehasa mashambani , ni jambo la kawaida wazazi
kuwaalika wazee wa jamii kuwapa majina watoto wanapozaliwa.
Mara nyingine chifu huwa anataka
kuiadhibu familia, anasema dereva, "au anafikiri kuwa mtoto aliyezaliwa ni
mzigo kwa familia."
Lakini kijana huyo si peke yake aliye na jina la
kutisha. Baadaye anakutana na "Chilumba", jina linalomaansiha
"kaburi la ndugu yangu"
Kisha anakutana na Balaudye -
"nitaliwa" na Chakufwa- "amekufa"
Pia anakutana na Daliso
linalomaanisha "baraka" na Chikondi linalomaanisa "upendo".
Kwenye utamaduni wa Afrika kuna
tabia ya kuwapa watoto majina kutokana na nyakati walizozaliwa, kwa mujibu wa
Clare Mulkenga afisa wa huduma za watoto nchini Zambia.
Anasema kuwa hata hivyo ni vyema
kwa wale wanaozaliwa nyakati nzuri lakini pia huwa ni bahati mbaya kwa wengine.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment