» » Aliyekuwa rais Korea Kusini Park Geun-hye 'kukamatwa'

Aliyekuwa rais Korea Kusini Park Geun-hye 'kukamatwa'

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionBi Park ndiye rais wa kwanza aliyechaguliwa Korea Kusini kuondolewa madarakani

Waendesha mashtaka wamesema wataomba idhini ya kumkamata aliyekuwa rais wa taifa hilo Park Geun-hye, kwa mchango wake katika kashfa ya ulaji rushwa nchini humo.

Alipoteza kinga ya rais dhidi ya kfuunguliwa mashtaka mapema mwezi huu na akaondolewa rasmi madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kudumisha uamuzi wa bunge wa kumng'oa madarakani.

Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa.

Bi Park amekanusha madai hayo.

Rais wa Korea Kusini awatelekeza mbwa wake ikuluWabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini

Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.

Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".

Wanasema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ukaharibiwa iwapo Bi Park hatakamatwa.

Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza.

Park aling'olewa vipi madarakani?

Bi Park aliondolewa madarakani kutokana na uhusiano wake wa karibu na Bi Choi.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionBi Choi (kati) ametuhumiwa kujihusisha katika ulaji rushwa

Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo kushinikiza kampuni kutoa mamilioni ya dola kama mchango kwa nyakfu za kusaidia jamii ambazo alikuwa anazisimamia.

Kaimu mkuu wa kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung, Lee Jae-yong, alikamatwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Bi Park, 65, anadaiwa kuhusika moja kwa moja katika hili, na kwamba alimruhusu Bi Choi uhuru wa kiwango kisichokubalika wa kufikia nyaraka rasmi za serikali.

Mada zinazohusiana

Korea KusiniSiasaUfisadi

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...