Hong Kong yamchagua
kiongozi mpya wa kwanza mwanamke
·
Carrie Lam amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa Hong Kong, akiwa
ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.
Bi Lam mwenye umri wa miaka 59 aliungwa mkono na serikali ya
China na alitarajiwa sana kushinda,
Hong Kong ina uhuru kutoka China lakini maandano yamekuwa
yakiongezeka kupinga uingiliajia wa China.
Kiongozi wa Hong Kong hachaguliwi na wananchi bali kamati ya
watu 1200 iliyo na watu wengi wanaoipendelea China.
Makundi ya kupigania demokrasia yamekuwa yakifanya maandamano
nje ya eno kulikofanyika uchaguzi huo na kuutaja kuwa usio wa haki.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionCarrie Lam akishangilia ushindi
Mshindani mkuu wa Bi Lam ambaye ni mkuu wa zamani wa masuala ya
uchumi John Tsang, alikuwa akipendelewa na watu kwa mujibu wa kura ya maoni.
Mgombea wa tatu alikuwa ni jaji mstaafu Woo Kwok-hing.
Bi Lam alipata kura 777 huku Tsang akipata kura 365 na Woo kura
21.
Wito wa kufanyika kwa uchaguzi huru umeshindwa licha ya
kushuhudiwa maandamano makubwa.
Kamati ya uchaguzi mjini Hong Kong ilimchagua Bi Lam kuchukua
mahala pa kiongozi wa sasa CY Leung, ambaye ataondoka madarakani mwezi Julai.
http://www.bbc.com/swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment