» » Raia wa Ufaransa wamtaka 'Obama kuwania urais nchini humo'

Raia wa Ufaransa wamtaka 'Obama kuwania urais nchini humo'

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMabango yalio na picha ya Obama yamewekwa mjini Paris

Ombi la mtandao la kumtaka Barrack Obama kuwania urais katika uchaguzi mkuu nchini Ufaransa limewavutia takriban wafuasi 42,000.

Mabango ya kampeni yanayosomeka ''Oui, on Peut'' ikimaanisha kauli mbiu ya kmpeni ya Obama ''Yes we can'' yametumika mjini Paris.

Bwana Obama sio raia wa Ufaransa hivyobasi hawezi kugombea urais.

Lakini wale wanaofanya mzaha huo wanasema kuwa lengo lao ni kuonyesha kwamba hakuna wagombea wazuri .

Ujumbe wao kwa wagombea hao kama alivyosema mmoja ya waandalizi wa ombi hilo ni ''jamani hamufai'.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionBango la aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama

Wapiga kura wa Ufaransa watashiriki katika uchaguzi mkuu mnamo tarehe 25 mwezi Aprili na iwapo wagombea hawatapata asilimia 50 ya kura katika raundi ya kwanza basi wapiga kura watarudi tena mnamo tarehe 7 mwezi Mei ili kuamua kati ya wagombea wawili waliopata kura nyingi.

Mgombea mwenye umaarufu katika uchaguzi huo ni Marine Le Pen ambaye amenufaiki na shutuma zinazomkabili mpinzani wake Francois Fillon tangu mwezi Januari hatua iliomfanya hakimu mmoja kusema kuwa ataanzisha uchunguzi kuhusu madai hayo.

Kura mbili za maoni zinamuonyesha Marine Le pen akiongeza dhidi ya Fillion lakini inasemekana kwamba wapinzani wake wanaweza kumshinda iwapo itafikia awamu ya pili ya uchaguzi.

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...