Polisi Afrika Kusini wamempata mtoto aliyetoweka
Polisi nchini Afrika Kusini wanasema kuwa mtoto mchanga aliyekuwa ametekwa nyara ndani ya gari la mamake siku ya Ijumaa mjini Durban, amepatikana akiwa hai.
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na uhalifu huo.
Msemaji wa polisi katika eneo la KwaZulu-Natal Luteni-Kanali Thulani Zwane, amethibitisha kuwa mtoto huyo alipatikana usiku wa manane kuamkia Jumapili.
Polisi walikuwa wakifuatilia vidokezo, ambapo baadaye viliwafanya kumpata ndani ya gari lililokuwa limeegezwa nje ya jumba la Mariannhill Toll Plaza.
Mtoto huyo wa mwezi mmoja anafahamika kama Siwaphiwe Mbambo.
Tangu siku ya Ijumaa polisi wakuwa wakimtafuta mtoto mmoja aliyetoweka, baada ya gari la familia yao kutekwa nyara katika eneo la Durban.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja, Siwaphiwe Mbambo, alikuwa katika kiti cha nyuma cha gari la mamake, pale gari hilo lilipotekwa na wanaume wawili waliokuwa na silaha nje ya duka moja kubwa la kununua bidhaa.
Mamake alimnyakuwa mwanawe wa kiume wa miaka minane, lakini majambazi hao walitoweka kwa kasi na gari hilo, huku mtoto huyo mchanga Siwaphiwe, akiwa ndani.
Gari hilo lilipatikana baadaye na maafisa wa polisi bila ya mtoto huyo.
Zaidi ya maafisa 100 wa polisi wamekuwa wakiendesha operesheni kali ya kumtafuta mtoto huyo, katika kampeini inayoendeshwa na vyombo vya habari ya mtoto kuibiwa nchini humo.
Watekaji nyara hao waliliendesha gari hilo kwa kasi, huku mtoto huyo mdogo akiwa bado ndani, maafisa wamesema.
Gari jeupe aina ya Toyota Yaris, lilipatikana, lakini mtoto huyo hakuwa amepatikana.
Msemaji wa polisi Thulani Zwane, awali alisema kuwa operesheni ya kumsaka mtoto huyo, inayohusisha maafisa wa polisi pamoja na kitengo cha mbwa wa kunusa, ulikuwa ukiendelea hadi msichana huyo mdogo apatikane.
"Jukumu letu la kwanza ni kumpata mtoto huyo," Bw Zwane alisema.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment