» » Angela Merkel aahirisha mkutano wake na Trump Marekani

Angela Merkel aahirisha mkutano wake na Trump Marekani


Josephine Shaw Lowell Memorial Fountain Bryant Park, New York City, 13 March 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKuna baridi kali katika jiji la New York
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahirisha safari yake ya kwenda Washington kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump kutokana na hali mbaya ya hewa.
Maeneo ya kaskazini mashariki mwa Marekani yanakabiliwa na kimbunga kikali.
Katika majimbo ya New York na New Jersey tayari yametangaza hali ya hatari huku upepo mkali wa majira ya baridi, ambao umeambatana na theluji ukiendelea kuvuma maeneo hayo.
Shule zimefungwa na safari za maelfu ya ndege kuahirishwa.
Kimbunga hicho kimepewa jina Stella na kinavuma kwa kasi ya hadi kilomita 100 kwa saa (maili 60 kwa saa).
Kuna uwezekano wa kimbunga hicho kutatiza wasafiri maeneo ya kaskazini mashariki mwa Marekani mapema Jumatano asubuhi, watabiri wa hali ya hewa wanasema.
Wakati mmoja, theluji ilikuwa ikimwagika kwa kasi ya hadi inchi 1-3 (sentimeta 2.5-7.6) kwa saa, kwa mujibu wa Alan Dunham mtaalamu wa hali ya hewa anayehudumu Taunton, Massachusetts.
Angela Merkel na TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Safari hiyo ya Merkel ambayo awali ilipangiwa kufanyika Jumanne sasa imepangiwa kufanyika Ijumaa.
Upepo huo pia umemlazimu waziri mkuu wa eneo la Taoiseach la Ireland Enda Kenny kusitisha ziara yake fupi kwenda Boston na badala yake akatumia treni hadi Washington.
Matrekta yamewekwa tayari kuondoa theluji barabarani Brooklyn, New YorkHaki miliki ya pichaAP
Image captionMatrekta yamewekwa tayari kuondoa theluji barabarani Brooklyn, New York
More than 6,500 flights have been cancelled, tracking service
Shirika la FlightAware limesema safari za ndege 6,500 zimeahirishwa New York, Washington, Boston, Baltimore na Philadelphia .
Shule zilifungwa Jumanne katika maeneo ya New York, Providence, Rhode Island na miji mingine kadha Massachusetts na Connecticut.
Fort Lee, N.J., Monday, March 13, 2017.Haki miliki ya pichaAP
Image captionWasafiri New Jersey wametahadharishwa kuhusu hali mbaya ya hewa
Gavana wa New Jersey Chris Christie pia ametangaza hali ya hatari na kuwataka watumishi wa umma ambao hawahusiki katika shughuli za dharura kusalia manyumbani.
Upepo mkali wa baridi kawaida hufuata kipindi cha joto la kadiri kaskazini mashariki mwa Marekani, lakini Februari iliyopita ulitajwa kuwa mwezi wenye kiwango cha juu zaidi cha joto tangu 1895 maeneo hayo.

Mada zinazohusiana


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...