Polisi wapambana na raia wa Uturuki, Uholanzi
Maafisa wa polisi wa kupambana na fujo nchini Uholanzi, wametumia michirizi ya maji, kuwatawanya waandamanaji wa Uturuki, waliokuwa wakifanya ghasia katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Rotterdam.
Waziri mkuu wa nchi hiyo, Mark Rutte, ameelezea ziara ya Waziri wa maswala ya Familia wa Uturiki kuzuru Uholanzi kuhutubia mkutano wa kisiasa, kama uliokosa uwajibikaji.
Waandamanaji hao walikuwa wakipinga hatua ya Uholanzi ya kuzima mkutano wa kisiasa, kuhusiana na kura ya maoni ya kuuendeleza utawala wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdowan utakaofanyika mwezi ujao wa Aprili.
Waziri wa maswala ya Familia wa Uturuki alikuwa amefika nchini humo, ili kuwahutubia raia wa Uturuki walioko Uholanzi, lakini mkutano huo ukatawanywa na maafisa wa polisi ambao walimsindikiza hadi mpakani mwa Ujerumani.
Ameelezea hatua hiyo ya polisi kama ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu na demokrasia.
Tayari utawala wa Uholanzi, ulikuwa umepiga marufuku mkutano huo, kwa sababu ya kiusalama, huku wakimzuia waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uturuki kusafiri nchini humo, ili kuhudhuria mkutano huo.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment