Bashar al-Assad: Syria kushirikiana na Marekani
Image captionRais Bashar al-Assad wa Syria
Rais Bashar al-Assad wa Syria ameelezea ahadi ya Rais Trump, kulishinda kundi la Islamic State, kwamba inatia moyo.
Akizungumza kwenye televisheni, Rais Assad alisema, kimsingi, kuna uwezekano wa kushirikiana, baina ya serikali yake na serikali mpya ya Marekani.
Mapigano yaanza upya SyriaPacha waliojeruhiwa Syria wafarikiUN:Mapigano yasitishwe SyriaSyria kumaliza mapigano
Lakini alisema, kitu kama hicho hakikupata kutokea kabla, na alielezea kuwepo kwa wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria, kwamba ni uvamizi.
Wakati wote wa vita vya miaka 6, Marekani imekuwa upande wa makundi yanayoipinga serikali ya Rais Assad.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment