» » Mwana wa Tshisekedi kuongoza upinzani DRC


Mwana wa Tshisekedi kuongoza upinzani DRC

AFPFelix Tshisekedi kuongoza upinzani DRC

Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo umemteua mwana wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa muungano huo Etienne Tshisekedi, ili kumrithi babake.

Felix Tshisekedi atakuwa rais wa muungano wa vyama tisa vinavyompinga rais Joseph Kabila.

Uteuzi wake ulitangazwa licha ya pingamizi kutoka kwa makundi mawili kwenye muungano huo.

Kiongozi wa muda mrefu wa muungano huo Etienne Tshisekedi, alikuwa ameuongoza kwenye mazungumzo ya mwezi Disemba kuhusu wadhifa wa urais.

Je, Etienne Tshisekedi ni nani?Malumbano kuhusu mazishi ya Tshisekedi yazuka DRCJe, kifo cha Tshisekedi kitaathiri mazungumzo ya amani DR Congo?

Kwenye makubaliano yaliyoafikiwa, bwana Kabila ataondoka madarakani baada ya uchaguzi ambao utafanyika mwaka huu.

Muhula wake wa pili madarakani ulikamilika rasmi Disemba iliyopita.

Kifo cha bwana Tshisekedi kilizua ghasia za mwezi mmoja kati ya wafuasi wake na vikosi vya usalama mjini Kinshasa, na kusababisha taharuki ndani ya upinzani.

REUTERSEtienne Tshisekedi alifariki mwezi mmoja uliopita

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...