» » Democrats wamtaka mwanasheria mkuu kujiuzulu Marekani

Democrats wamtaka mwanasheria mkuu kujiuzulu Marekani

Image captionMwanasheria mkuu wa Marekani Jeff Sessions

Wanachama wa chama cha Democrats nchini Marekani wanasema bado hawajashawishiwa na matamshi ya karibuni ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kuhusiana na mawasiliano yake na balozi wa Urusi 2016.

Kiongozi wa wabunge wa chama cha Democrats Nancy Pelosi anaongoza wito wa kiongozi huyo mkuu wa mashtaka nchini humo kujiuzulu.

Rais Donald Trump amesema kwamba Sessions ni mtu mwaminifu na kusema kuwa shinikizo ya wanachama wa Democrats ni ya kibinafsi.

Bwana Sessions awali alijiondoa katika uchunguzi wa shirika la FBI kuhusiana na hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Lakini amesema hakudanganya wakati aliposema kuwa hakuwasiliana na raia wa Urusi.

Image captionKiongozi wa wabunge wa chama cha Democrats Nancy Pelosi

Alisisitiza kuwa matamshi yake ni ya uaminifu na sawa kama alivyoelewa wakati huo.

Bwana Sessions alikuwa akizungumza baada ya kubainika kwamba alikutana na balozi wa Urusi Sergei Kislyaka mara mbili mwaka uliopita.

Bwana Sessions wakati huo alikuwa mwanachama wa kamati ya usalama katika baraza la seneti nchini humo.

Lakini tayari alikuwa mwanachama maarufu wa kundi la kampeni ya bwana Trump.

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...