Marekani yapinga pendekezo la China kuhusu K. Kaskazini
Image captionBalozi wa Marekani Nikki Halley amesema kuwa njia tofauti za kukabiliana na Korea Kaskazini zimewekwa wazi
Maafisa wa Marekani wamepinga pendekezo kwamba Korea Kaskazini itasitisha majaribio ya makombora yake na yale ya Kinyuklia iwapo Marekani itasitisha vitendo vyake katika eneo hilo.
Idara ya maswala ya kigeni nchini humo imesema kuwa mpango huo hautasaidia huku balozi wa Umoja wa Mataifa akisema kuwa Korea Kaskazini haifikirii.
Korea Kaskazini yasema China ni kibaraka wa MarekaniNdege za kivita za Marekani zapaa KoreaChina: Marekani itatue mgogoro wake na Korea KaskaziniMarekani yapeleka mfumo wa ulinzi K.Kusini
Pendekezo hilo la China linajiri baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora yake manne ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya kimataifa.
Wakati huohuo, Marekani imeanza kupeleka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Pia inaendela na mazoezi ya pamoja na wanajeshi wa Korea Kusini hatua inayokasirisha Korea kaskazini.
Haki miliki ya pichaAPImage captionMajaribio ya makombora yaliofanywa na Korea Kaskazini yakionyeshwa katika runinga
Waziri wa maswala ya kigeni nchini China Wang Yi alisema siku ya Jumatano kwamba hali hiyo ni sawa na treni mbili zinazokaribiana kugongana ana kwa ana baada ya moja kati yazo kukataa kuipisha nyengine.
Usitishwaji wa operesheni za kijeshi na pande zote mbili unaweza kupunguza hali ya wasiwasi na kufungua mazungumzo alisema.
Lakini msemaji wa idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani Mark Toner alisema kuwa hilo ni sawa na kufananisha ''tufaa na chungwa''.
''Kile tunachofanya kama ushirikiano wetu kujilinda na Korea Kusini ni tofauti na ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Korea Kaskazini''.
Lakini amesema kuwa Marekani inafaa kuangalia mbinu nyengine za kukabiliana na Korea kaskazini.
''Juhudi zote tulizofanya kujaribu kulishawishi taifa la Korea Kaskazini kufanya majadiliano zimegonga mwamba.
''Kwa hivyo tunafaa kuangalia mbinu mpya za kulishawishi taifa hilo kuona kwamba ndilo litalalofaidika''.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment