» » Magufuli hajaagiza Wakenya wafukuzwe Namanga

Tanzania: Magufuli hajaagiza Wakenya wafukuzwe Namanga

Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpyaSambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako

Haki miliki ya pichaAFPImage captionSerikali ya Tanzania imesema inawafukuza wageni wasio na vibali vya kuishi Tanzania

Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikienea katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Rais Magufuli aliamuru Wakenya wanaoishi upande wa Tanzania katika mji wa mpakani wa Namanga watimuliwe.

Tanzania imeiomba serikali ya Kenya kupuuzilia mbali taarifa hizo na badala yake, nchi hizo mbili "ziangazie kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kibiashara ambao umekuwepo."

Taarifa hizo zilisababisha maandamano na vurugu katika mji huo mapema wiki hii, Wakenya wakilalamika.

Shughuli za kiserikali na za kibiashara katika mji huo zilitatizwa na vurugu hizo, sana Jumatatu.

Utulivu warejea Namanga, mpakani mwa Kenya na TanzaniaMagufuli: Kenya ni mshirika wetu nambari moja Afrika

Katibu katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Aziz Mlima amesema taarifa hizo ni za uongo.

Alisema lengo la taarifa hizo ni "kumharibia Rais Magufuli sifa zake nzuri ambazo amejizolea kufikia sasa pamoja na picha nzuri ya Tanzania kwa jumla."

Dkt Aziz hata hivyoa amesema sheria za uhamiaji ni sharti zifuatwe.

Amesema wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilifanya operesheni ya kuwatimua wageni, wakiwemo Wakenya, wanaoishi Tanzania bila vibali vya kuishi au kufanyia kazi nchini humo.

Image captionWaandamanaji walitatiza shughuli katika mji huo wa mpakani Jumatatu

Mada zinazohusiana

MagufuliKenyaTanzania

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles