» » Kazuyoshi Miura wa Japan awa mchezaji mzee zaidi kufunga bao katika

Kazuyoshi Miura wa Japan awa mchezaji mzee zaidi kufunga bao katika soka

Haki miliki ya pichaREX FEATURESImage captionKazuyoshi Miura alifunga mabao mawili mechi 20 alizocheza msimu uliopita, nyingi akiingia kama nguvu mpya kipindi cha pili

Raia wa Japan wa umri wa miaka 50 ameweka rekodi mpya ya kuwa mtu wa umri mkubwa zaidi kufunga bao katika mechi ya soka ya ushindani.

Kazuyoshi Miura aliweka rekodi hiyo kwa kufunga bao la pekee wakati wa ushindi wa 1-0 wa Yokohama FC dhidi ya Thespa Kusatsu katika ligi ya daraja la pili nchini Japan.

Rekodi ya awali iliwekwa mwaka 1965 na Mwingereza Stanley Matthews, aliyefunga bao lake la mwisho mechi ya ushindani akiwa na umri wa miaka 50 na siku tano.

Miura anamzidi umri kwa siku tisa.

Babu atafuta klabu mpya ya kuchezeaJicho la mchezaji latoka akiwa uwanjani

Miura, ambaye aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Japan na kuwafungia mabao 55 katika mechi 89, kwa sasa anacheza soka msimu wake wa 32.

Alistaafu soka ya kimataifa miaka 17 iliyopita.

Miura wakati mmoja alicheza soka ya kulipwa Ulaya.

Alianza uchezaji wake akichezea Santos ya Brazil na akacheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa mwaka 1986.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionKazuyoshi Miura alianza kuchezea Santos ya Brazil mwaka 1986

Alichezea Genoa na Dinamo Zagreb miaka ya 1990.

Mada zinazohusiana

JapanMichezo

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...