CUF YAIGARAGAZA CCM UCHAGUZIWASERIKALI ZA MTAA WILAYA YA LINDI
Wakati Chama Cha Wananchi-CUF kikiwa katika mgogoro wa uongozi ngazi ya taifa, kimeonyesha kutotetereka katika ngazi zake za chini na wananchi wamendelea kuwa na imani nacho. Chama hicho kimebuka na ushindi mnono katika uchaguzi wa kuziba nafasi wazi za wenyeviti wa mitaa katika halmashauri ya manispaa ya Lindi. Baada ya kuzoa viti vyote saba vilivyokuwa vinashindaniwa.
Akitangaza kwa naiba ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Lindi, matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana. Ofisa uchaguzi wa manispaa ya Lindi, Emmanuel Lweyo, alisema katika uchaguzi huo ni vyama vya siasa vya CCM na CUF pekee ndivyo vilivyo weka wagombea. Ofisa uchaguzi huyo alitaja matokeo hayo kama ifutavyo:
Majina ya wagombea, idadi ya kura za kila mmoja, jina la mtaa , kata kwenye mabano na chama. Mtaa wa Migombani (Mwenge). Mshindi ni Salima Ahmad wa CUF aliyepata kura 136 dhidi ya 133 alizopata Lucas Makundi wa CCM, Mtaa wa sabasaba (Nachingwea), Hamza Mohamed wa CUF alishinda kwa kura 189 dhidi ya 142 alizopata Edna Mtambo wa CCM, mtaa wa Mnubi (Mitandi) Fatuma Mbaruku aliibuka mshindi baada ya kupata kura 136 dhidi ya 75 alizopata mgombea wa CCM, Rahibu Kaisi. Mitaa mingine ni Tulieni(Sabasaba) mshindi ni Fadhili Makwinya kwa kura 141 dhidi ya 38 alizopata Mary Edwin wa CCM, mtaa wa Narunyu(Tandangongoro) Rashidi Lichuma alishinda kwa kura 50 dhidi ya 38 za Nassoro Karim wa CCM, Ndoro juu(kata ya Ndoro) Mzee Karibu Bao alishinda kwa kura 121 dhidi ya 95 za Paulina Kanyusi wa CCM na RahaleoB (Mingoyo) Shaibu Mwizagu alisahinda kwa kura 209 dhidi ya 176 za Hafa Hamisi wa CCM.
Akizungumzia matokeo hayo mkurugenzi wa mipango na uchaguzi wa CUF wilaya ya Lindi, Is-haka Mchinjita alisema licha ya mshikamano na umoja wanachama na wapenzi wa chama hicho lakini pia ushirikiano ulioneshwa na UKAWA umechangia ushindi huo kihistoria katika manispaa ya Lindi. Mchinjita alisema mwitikio mkubwa ulioneshwa na wananchi katika mikutano ya kampeni na siku ya kupiga kura umedhihirisha wananchi wanazitambua haki zao na wanahitaji mabadiliko.
“Ingawa kuna mgogoro wa uongozi ngazi ya taifa lakini matokeo aya yanaonesha wananchi na wanachama wanaendelea kuwa na imani na chama chetu, lakini nalishukuru pia jeshi la polisi kwa kutenda haki na kutekeleza majumu yake kikamilfu katika kipindi chote,” alisema Mchinjita.
Nae naibu meya wa manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto aliwataka viongozi hao waliochaguliwa watimize ahadi walizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni. Pia wasimamie, wahimize shuguli za maendeleo na wawatetee wananchi ambao katika uchaguzi huo wameonesha imani kwao na chama.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi, Muhsin Ismail licha ya kusema yeye sio msemaji wa chama, lakini alisema wamekubali matokeo. Wanajipanga kufanya vizuri na kushinda kwa ushindi mkubwa katika chaguzi zijazo.
___________________________________________________
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment