» » Hatma ya Joe Hart kusubiri Manchester City Hatma ya Joe Hart kusubiri Manchester City posted about 1h ago 1-03-2017 9:56 Michezo Mlinda lango namba moja wa timu ya Taifa ya Uingereza, Joe Hart huenda akaondoka Manchester City mwishoni mwa msimu atakapokuwa amemaliza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Torino ya Italia. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekataa kuzungumzia hatma ya mchezaji huyo hadi mwishoni mwa msimu. Guardiola hajavutiwa na Joe Hart tangu ajiunge na Manchester City na aliamua kumsajili Claudio Bravo kutoka FC Barcelona na kumtoa Hart kwa mkopo kwenda klabu ya Torino inayoshiriki Serie A. Hata hivyo Bravo(33) ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa na Guardiola hivyo siku za karibuni amejikuta akimtumia zaidi Willy Caballero aliyetarajiwa kuwa msaidizi wake. Mkataba wa Caballero(35) unaisha mwishoni mwa msimu lakini Manchester City bado haijafanya nae mazungumzo hivyo kuashiria kuwa huenda klabu hiyo ina mpango wa kusaka mlinda mlango mwingine. Sambamba na Caballero, Yaya Toure na Bacary Sagna nao mikataba yao inakamilika mwishoni mwa msimu na hakuna mazungumzo ya kuwaongeza mikataba mipya. Wote wameambiwa wasubiri mpaka mwishoni mwa msimu.

Hatma ya Joe Hart kusubiri Manchester City



Hatma ya Joe Hart kusubiri Manchester City

  • posted about 1h ago
  •  
  • 1-03-2017 9:56
  •  
  • Michezo
  • Mlinda lango namba moja wa timu ya Taifa ya Uingereza, Joe Hart huenda akaondoka Manchester City mwishoni mwa msimu atakapokuwa amemaliza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Torino ya Italia.

    Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekataa kuzungumzia hatma ya mchezaji huyo hadi mwishoni mwa msimu.

    Guardiola hajavutiwa na Joe Hart tangu ajiunge na Manchester City na aliamua kumsajili Claudio Bravo kutoka FC Barcelona na kumtoa Hart kwa mkopo kwenda klabu ya Torino inayoshiriki Serie A.

    Hata hivyo Bravo(33) ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa na Guardiola hivyo siku za karibuni amejikuta akimtumia zaidi Willy Caballero aliyetarajiwa kuwa msaidizi wake.

    Mkataba wa Caballero(35) unaisha mwishoni mwa msimu lakini Manchester City bado haijafanya nae mazungumzo hivyo kuashiria kuwa huenda klabu hiyo ina mpango wa kusaka mlinda mlango mwingine.

    Sambamba na Caballero, Yaya Toure na Bacary Sagna nao mikataba yao inakamilika mwishoni mwa msimu na hakuna mazungumzo ya kuwaongeza mikataba mipya.

    Wote wameambiwa wasubiri mpaka mwishoni mwa msimu.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...