» » Rais Trump aapa kufufua ari na bidii ya Wamarekani

Rais Trump aapa kufufua ari na bidii ya Wamarekani


Rais Trump akitoa hotuba yake katika bunge la Congress nchini Marekani
Image captionRais Trump akitoa hotuba yake katika bunge la Congress nchini Marekani
Rais Donald Trump amehutubia wabunge wa Marekani muda mfupi uliopita ambapo ameahidi kufufua nguvu na bidii ya Wamarekani.
Amesema kwa muda mrefu, Wamarekani wa kipato cha kati wamekuwa wakipungua na miundo mbinu imedorora, huku maovu kama vile Uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya kupitia mipaka ya Marekani yakiendelea kushamiri.
Bwana Trump amesema ataiomba bunge kuidhinisha bajeti ya dola trilioni moja kwa lengo la kuwekeza katika miundo mbinu ya taifa hilo.
Ameahidi kupunguza kodi inayotozwa kampuni za Marekani, na pia kupunguza kodi kwa Wamarekani wa kipato cha kati.
Aidha Aidha rais Trump amesema kwamba atabadilisha mfumo wa uhamiaji ulioko sasa ambapo watu walio na ujuzi wa chini wanaruhusiwa kuingia Marekani, na kusema kwamba wahamiaji wanaoonekana kwamba wana ujuzi wa hali ya juu na wanastahili kuingia Marekani, wataruhusiwa.
Anasema kazi yake si kulinda ulimwengu, bali ni kulinda Marekani.
Amsema ataunga mkono muungano wa mataifa yanayojihami ya NATO.
Amesisitiza kwamba Marekani itafanya kazi na washirika wake kuangamiza kundi la kigaidi la Islamic state.
Wakati wabunge wa Republican wakishangilia na kufurahia hotuba hiyo, wabunge wa democrat waliketi kimya bungeni, na baada ya hotuba kukamilika, mmoja wao akasema hotuba ya Trump haikuwa ya kuunganisha.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...