» » Brazil yafuzu Kombe la Dunia 2018 baada ya kulaza Paraguay

Brazil yafuzu Kombe la Dunia 2018 baada ya kulaza Paraguay


NeymarHaki miliki ya pichaAP
Image captionBrazil wamefunga mabao 24 na kufungwa mawili pekee mechi zao nane za karibuni za kimataifa
Brazil imekuwa taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia ambazo zitachezewa nchini Urusi mwaka ujao.
Walifuzu baada ya kulaza Paraguay 3-0, nao Argentina na Uruguay wakashindwa.
Hii ina maana kwamba sasa Brazil hawaweza kumaliza chini ya nafasi nne miongoni mwa mataifa ya Amerika Kusini, ambapo mataifa ya kwanza manne ndiyo hufuzu.
Brazil waliwashinda Paraguay kupitia mabao ya mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar na mchezaji wa Real Madrid Marcelo.
Neymar pia alipoteza mkwaju wa penalti.
Brazil kwa sasa wamo alama tisa mbele ya Colombia ambao wanashikilia nafasi ya pili.
Huo ulikuwa ushindi wa nane kwa Brazil chini ya Tite.
Paraguay, wamo alama chini ya nne bora, zikiwa zimesalia mechi nne kuchezwa.
Argentina wanakabiliwa na kibarua kufuzu baada ya kushindwa 2-0 na Bolivia na kushuka hadi nambari tano, alama moja nyuma ya Chile.
Uruguay, waliochapwa 2-1 na Peru mjini Lima Jumanne, wamo nambari tatu.
Taifa litakalomaliza nafasi ya tano litacheza mechi mbili za muondoano (nyumbani na ugenini) dhidi ya taifa kutoka Oceania.
Brazil celebrateHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBrazil wamo alama 11 mbele ya Argentina

Mada zinazohusiana

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles