» » Messi apigwa marufuku mechi nne kwa kumtukana mwamuzi

Messi apigwa marufuku mechi nne kwa kumtukana mwamuzi


Lionel MessiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMessi alionekana kukerwa na uamuzi wa kumwadhibu dakika za mwisho za mechi dhidi ya Chile
Nyota wa Argentina Lionel Messi amepigwa marufuku mechi nne za kimataifa kwa kumtukana mwamuzi msaidizi wakati wa mechi kati ya taifa lake na Chile siku ya Alhamisi mjini Buenos Aires.
Shirikisho la soka duniani FIFA, lilitangaza uamuzi huo saa chache kabla ya Argentina kukutana na Bolivia katika mechi muhimu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.
Argentina, walionekana kumkosa sana mshambuliaji huyo wa Barcelona, na walilazwa 2-0 katika mechi hiyo iliyochezewa mji wa La Paz.
Mabao ya Bolivia yalifungwa na Juan Carlos Arce na Marcelo Martins.
Argentina wanakabiliwa na hatari ya kushindwa kufuzu kwa michuano hiyo itakayoandaliwa nchini Urusi.
Timu nne za kwanza Amerika Kusini ndizo huhakikishiwa nafasi ya kucheza michuano hiyo.
Kwa sasa, Argentina wanashikilia nafasi ya nne.
Zikiwa zimesalia mechi nne za kufuzu, Colombia walipanda juu ya Argentina na Uruguay na kutua nafasi ya pili kwa kulaza Ecuador 2-0 kupitia mabao ya James Rodriguez na Juan Cuadrado.
Argentina huenda wakatolewa nafasi ya nne iwapo Chile watafanikiwa kuwalaza Venezuela baadaye.
Uruguay watakuwa pia uwanjani dhidi ya Peru nao Brazil wanaoongoza wakutane na Paraguay.
Bolivia washerehekeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBolivia wameshinda mechi tatu pekee kati ya 14 walizocheza za kufuzu Kombe la Dunia
Ramiro Funes MoriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRamiro Funes Mori aliumia kwenye goti mechi hiyo dhidi ya Bolivia

Mada zinazohusiana

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles