» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: TABIA ZA AJABU-SEHEMU YA PILI (2)


USHINDI HATIMAYE- TABIA ZA AJABU-2
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
WADHAMINI: Chama cha Wajasiriamali na Wanataalum(ATAPE) wakishirikiana na Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini.
Mafungu:1 Samwel 25:23-32;Ufunuo 17:3-5;2Korinth 11:12; Yerem 31:32; Terem 51:6,7; Math 15:9; Mwanz 11:4,7,9 ;Yerem 3:20
Tabia nyingine za ajabu ni pale mwanadamu anapoacha kuisikiliza sauti ya Mungu,kufuata mafundisho potofu na ibada bandia kinyume na maelekezo ya Mungu.Je unapigana vita vya nani? Vita vya wanadamu! Ikiwa unapigana vita vya Bwana kuna ushindi hatimaye.
Babeli hutokana na jina lile la zamani la Babeli, maana yake machafuko. Katika Biblia jina hili humaanisha machafuko ya kidini, kutokana na aina mbalimbali za mafundisho. Katika Ufunuo 17 jina hili Babeli husimama badala ya mwanamke, ambaye kimaandiko Matakatifu ni kanisa. Bikira safi hufananishwa na kanisa takatifu. Mwanamke mchafu hufananishwa na kanisa potofu lililoasi, katika Biblia uhusiano baina ya Kristo na kanisa hufananishwa na ndoa.
Neno la Mungu ni kweli na Uzima,huwezi kumpendeza Mungu kwa kudai tu kwamba unamwamini. Kwani, Biblia inasema kwamba hata roho waovu wanaamini kwamba Mungu yuko.Hata hivyo, ni wazi kwamba hawafanyi mapenzi ya Mungu na hawana kibali chake. Ili tukubaliwe na Mungu, haitoshi tu kuamini kwamba yeye yuko, ni lazima tufanye mapenzi yake.
Ni lazima pia tujitenge kabisa na dini za uwongo,mafundisho bandia na kukubali ibada ya kweli maana Mungu harekebishwi na mwanadamu. Kinyume na Mungu hakuna aliyewahi kupambana na Mungu akashinda vita. Mungu akiendesha gari lako funga mdomo utafika salama; au unaupiga ngumi mchokoo?
Ufunuo 17:5 Biblia inaonyesha kwamba dini zote za uwongo ni sehemu ya Babeli Mkuu, Babeli ya zamani ni mahali ambako dini za uwongo zilianzia baada ya gharika. Mafundisho na mazoea mengi ambayo ni ya kawaida katika dini za uwongo yalianza zamani huko Babiloni.
Wababeli waliabudu miungu lakini Biblia iko wazi kwamba kuna Mungu mmoja tu wa kweli, Yawe, na kwamba Yesu Kristo ni Mwana wake. Ibada ya Babeli ya zamani ilienea duniani pote,na hata leo inaweza kuenea ulimwenguni na kuitwa milki ya ulimwengu ya dini za uwongo. Na Mungu ametabiri kwamba milki hiyo ya dini za uwongo itaharibiwa ghafula..
Ni aina gana ya tabia ya ajabu(Babeli) umepitia,machafuko mwambie Yesu akusafishe.Kama ni maagizo ya wanadamu toka huko,njoo kwa Yesu,jitenge na kila aina ya Babeli ili mvinyo wa Babeli usikupate. Yawezekana baadhi ya watu wakaacha kushirikiana nawe kwa sababu ya uamuzi wako wa kuacha kushirikiana na dini ya uwongo,shikilia kwa BWANA. Ukitamtambua Mungu wa kweli mpe heshima yake ili uwe MSHINDI HATIMAYE.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...