» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: TABIA ZA AJABU SEHEMU YA TATU (3)

USHINDI HATIMAYE- TABIA ZA AJABU-3
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga  
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
Mafungu: Mwz 10:8-12,Yerem 51:6,7;Ezekiel 8:13,14,Yeremia 7:17,18;Ezek 8:16,Ezek 22:6 ;Matendo 20:29-30
Miongoni mwa tabia za ajabu ni kukuta maandishi ya ajabu na wakati mwingine ni matusi kwenye mawe makubwa au madaraja,waweza fikiri kwamba huyu mtu alipokuwa anaandika alikuwa na akili timamu au namna gani.Lakini pia ajabu nyingine ni kuona mtu mzima akila kizibo cha kalam,ambapo wataalam husema kwamba mtu huyo huenda kuna hatua ya makuzi katika utoto wake hakuipitia hasa ya kunyonya vidole.
Lakini katika maswala ya Imani kuna mtu aweza ng’ang’ania dini aliopo eti sababu kubwa alizaliwa akakuta wazazi wake wakiabudu huko haijalishi yuko katika ibada sahihi au namna gani,hiyo ni tabia ya ajabu.Ni mpango wa shetani kuendelea kuabudiwa na kuabudu miungu kwa ufundi mkubwa na ibada za kusisimua ili kuficha ukweli lakini ni kiini cha maovu ma kufuru kwa Mungu wa Mbinguni
Nimrod alikuwa mtu maarufu sana,ananenwa kuwa mtu hodari(Mwanzo 10:8-12).Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa ni Babeli, Akadi, Ereku, Kalne na Ashuru; mkewe alikuwa akiitwa Shemiramis.Unaweza ukawa maarufu lakini hujui kitu,mafundisho potofu yanalevya,ibada potofu inalevya.Chuja unacho kiamini nawe utakuwa mshindi kwa Bwana.
Baada ya miaka ya kifo cha Nimrod,malkia alizini na kuhani wake wa matambiko katika ibada ya jua kisha alibeba mimba, kwakuwa alikuwa malkia na hana mume,na huku ana mimba,watu wake walimuuliza kwamba hiyo mimba imetoka wapi na niyanani wakati huna mume? Alizaliwa Tamuzi ambaye aliaminika kwamba ni mtakatifu kwa kuwa mimba yake imetokana na mionzi ya jua na iliaminika kwamba Nimrod aliendelea kuzaa na mke wake huku akiwa katika jua na sherehe inaonekana ilifanyika katika kuzaliwa kwake TAMMUZ (Yeremia 7:17-18)
TAMMUZ ni Mungu jua, Je! Nyumba ya Bwana yawezaje kuwa na miungu?Imani yako ipime kwa biblia na si kwa kufuata wingi wa watu wanaoabudu.Wakati mwingine waweza kuwa katika Imani na miungu pasipo wewe kujua.Angalia Mungu anasema,Neno la Mungu linasema simama imara katika Kristo Bwana wetu.Ukweli una pimwa kwa ukweli wenyewe.
Ishtar ni lango kuu la kuingilia Babel.Neno “Easter”linatumika kwa lugha ya kiingereza ikimaanisha Pasaka ni neno lenye asili ya kutokana na neno “Ashtar” ambalo lilichukuliwa kutoka katika miungu na wakristo wa karuhusu kuingia kwa upagani makanisani.Imani potofu na zimetapakaa duniani lakini Mungu anatafuta Kanisa safi na kamilifu linalofuata maagizo ya Mungu katika Biblia. Kwa kufuata miungu na Imani potofu ni tabia ya ajabu ambayo kamwe Mungu hataivumilia.KUWA MWAMINIFU HATA KUFA NI USHINDI HATIMAYE.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...