» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: ADUI MWENYE HASIRA

USHINDI HATIMAYE- ADUI MWENYE HASIRA
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
WADHAMINI: Chama cha Wajasiriamali na Wanataalum(ATAPE) wakishirikiana na Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini.
Mafungu: 1Samwel 18:7-9; 1 Petro 2:9-10
“Sauli akakasirika sana; sehemu hii ya kurudia rudia ya wimbo huu ilimkasirisha sana. Akafikiri kuwa, “Wamempa Daudi makumi elfu, lakini mimi wamenipa elfu tu. Apate nini zaidi isipokuwa ufalme?” Kuanzia wakati ule na kuendelea Sauli akawa na jicho la wivu juu ya Daudi.”(1Samwel 18:8-9)
Unafanya nini unapokutana na adui tena mwenye gadhabu? Maarifa na hekima hutumika ili kumshinda adui. Hekima ni kinyume kabisa cha upumbavu, ujinga, na ukichaa. Kwa hiyo, Maandiko hutusihi tujipatie hekima. Adui akiwa na hasira ni ishara ya kushindwa.Adui yako halisi si mwanadamu bali ni SHETANI aitwaye IBIRISI.
Shetani alituonea wivu tangu siku ile tulipomtangaza KRISTO kama BWANA NA MWOKOZI wa maisha yako. MUNGU MWENYE NGUVU MFALME WA AMANI. Bwana anakufundisha vita mpaka uweze kupambana na kupata ushindi. Bwana anakufundisha vita kwa namna ya rohoni, anakuongoza nakukutia nguvu kuelewa namna ya kutumia silaha za rohoni.
Mungu hutufundisha mambo makuu na hayo mambo makuu atufundishayo hutufanya kugeuka na kuwa watu tofauti yaani watu wenye kumuheshimu Mungu ili aweze kutenda kazi pamoja nasi. Hakuna mtu yeyote aliyewahi kupitia magumu, kupitia vita huku akimtegemea Bwana katika vita yake naye Bwana alipomshindia akabakia kwenye ngazi ile ile.
Mungu hutukuzwa kupitia vita yako.Pale ambapo ulikuwa una matatizo, ulipokuwa unakabiliwa na vita kubwa ya kusemwa vibaya katika maisha yako ndipo hapo hapo Mungu hujitwalia utukufu. Kumbuka kuna HAKI ya KRISTO.Kumkubali Kristo unapata vazi la haki Yake. WEWE mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU. AMEN
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...