» » USHINDI HATIMAYE - SOMO: SIKU NGUMU SANA MAISHANI

USHINDI HATIMAYE - SIKU NGUMU SANA MAISHANI
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
WADHAMINI: Chama cha Wajasiriamali na Wanataalum(ATAPE) wakishirikiana na Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini.
MAFUNGU: 1 Samwel 21:1-9; Waruni 1:17; Warumi 3:10, Warum 6:23; 2 Petro 3:9; Mathayo 12:3-7; Kutoka 34:6, 7
Hofu haipaswi kuwa sehemu ya maisha ya muumini, jinsi gani mtu anaishinda wasiwasi? Mungu anatueleza tumpe woga wetu wote na wasiwasi. Kwa nini Mungu Anataka kutubebea matatizo yetu? ni kwa sababu Yeye(MUNGU) anatujali.
Sisi imetupasa kumpa Mungu matatizo yetu,ameahidi kutupa amani ipitayo uwezo wetu wote. lazima tulete mahitaji yetu yote na wasiwasi kwa Mungu katika maombi badala ya kujisumbua kwayo.Woga ukitawala utakusababisha kutumia njia zako mwenyewe maishani.
Kuna kuogopa endapo utasahau kule Mungu alikokutoa.Tusitumie juhudi zetu wenyewe ili kumpendeza Mungu.Je! utalipa nini ili usamehewe na Mungu? Tujifunze kwa Daudi ambaye aligundua amekosa,Msamaha ni bure. Woga unaondoka katika maisha yako kwa Yesu aliyekuja katika mwili. Yesu amemharibu Shetani aliyetutawala kwa woga wa mauti, Akatuacha huru.
Tambua dhambi zako,Mwite Yesu!Katika maisha watu wengi hukwama kutatua changamoto zao wanapokuwa kwenye hali ngumu za kimaisha,twapasa kupaza sauti kwa neno lolote TUSIKATE TAMAA ,bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu.
Kuruhusu kutawaliwa na woga, ni kumfanya Mungu kuwa na uwezo mdogo kuliko yale yanayotuogopesha.Hatupaswi kuyaogopa makumi elfu ya watu, waliojipanga juu yetu pande zote, TUSIKANYAGE VITU VITAKATIFU.MUNGU hapendi mtu yeyote apotee, akikusamehe anakupatia AMANI YA MOYO; BWANA AKUBARIKI
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...