» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: MAJIRA YA UKAME

USHINDI HATIMAYE- MAJIRA YA UKAME
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
WADHAMINI: Chama cha Wajasiriamali na Wanataalum(ATAPE) wakishirikiana na Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini.
Mafungu: kumbu 32:10;1Samwel 19:11-24; 1 korinth 14:33;1 korinth 14:1-4;mark 16:17;Matendo 2:1-3
“Katika nchi ya jangwa alimkuta, katika nyika tupu ivumayo upepo. Alimhifadhi na kumtunza; akamlinda kama mboni ya jicho lake.”(Kumb 32:10)
Kuna wakati inatokea una kiu na unayaona maji lakini si kila maji yafaa kunyweka. Wana wa Israel katika safari yao ya kutoka Misri na kwenda Kanaani. Walipofika sehemu panaitwa Refidimu wakawa na kiu ya maji maana hapo maji hayakupatikana.
Jangwa ni ishara ya dhambi ambayo inatutenga mbali na Mungu wetu. Unaweza ukawa katika jangwa la mateso ya umizimu,watu wengi wanapeleka shida zao kwa umizimu lakini mwisho wakaharibikiwa zaidi,jangwa la uchumi,ndoa yako ni migogoro,chuki,maseng’enyo,hasira,fitina,uhasherati, lakini ukimwita Yesu atasikia shida yako na kukutoa katika jangwa lako na kukupatia maji na usipate kiu tena.
Daudi alipitia katika ukame(changamoto) lakini alipomkumbuka BWANA,BWANA akamwangalia kwa macho ya upendo.Mwanadamu anaweza kufanikiwa wakati wa ukame ila anatakiwa kujua afanyaje ili aweze kushinda na kufanikiwa katikati ya magumu. Katika hali yeyote utakayo pitia Mungu atatokea, kila mara Mungu anapokutokea lazima hali ibadilike.
KUMWABUDU MUNGU KWA UTARATIBU- VIGEZO VYA KUNENA KWA LUGHA:
Kuna wakati majibu ya majangwa yetu yanajibiwa kupitia kufunga,kuomba na kutafakari NENO. Namna bora ya kumwabudu Mungu yaweza kututoa katika jangwa la kuwa mbali na Mungu.
1 korintho 14:22, 23, 27,28
“27.Kama mtu ye yote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu si zaidi, mmoja baada ya mwingine na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28Lakini kama hakuna mtu ye yote wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.”
Nguvu ya ROHO MTAKATIFU ni maji wakati wa ukame inaposhuka juu ya mtu, ni ishara ya kwamba mlango wa majira mapya umefunguliwa na ni wakati wa mtu kutulia mbele za BWANA ili kupata mwelekeo na kuanza utekelezaji wa kusudi la MUNGU. MUNGU hana chuki na wewe bali anakuwazia mawazo ya amani wala si mabaya. Anachukia zile dhambi zote ulizofanya au unazofanya lakini anakupenda wewe upeo mfungulie moyo wako ili apate kuingia na kutawala.
Kwa hisani ya kirumba adventsta
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...