» » Andy Puzder, aliyeteuliwa na Trump kuwa waziri ajitoa

Andy Puzder, aliyeteuliwa na Trump kuwa waziri ajitoa

Donald Trump na Andy PuzderHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAndrew Puzder ndiye wa kwanza aliyeteuliwa na Trump kukosa kuidhinishwa
Andrew Puzder, aliyekuwa ameteuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa waziri wa masuala ya wafanyakazi, amejiondoa muda mfupi kabla yake kuhojiwa na wabunge.
Puzder alipoteza uungwaji mkono wa maseneta kadha wa chama cha Republican baada yake kukiri kwamba alimwajiri mhamiaji aliyeingia Marekani kinyume cha sheria kuwa mjakazi.
Bilionea huyo pia amekosolewa kwa matamshi yake kuhusu wanawake na wafanyakazi katika migahawa yake.
Yeye sasa anakuwa mtu wa kwanza miongoni mwa waliopendekezwa na Trump kuwa waziri kukosa kuidhinishwa.
Talaka yake na mkewe mwaka 1980, ambayo ilikumbwa na mvutano mkubwa, pia imemwathiri.
Majuzi, ilibainika kwamba mke wake wa zamani, Lisa Fierstein, alishiriki kama mwathiriwa wa udhalilishaji kwenye ndoa katika kipindi cha Oprah Winfrey mwaka 1990 ambacho kilifahamika kwa jina High Class Battered Women (Wanawake wa tabaka la juu wanaopigwa na waume zao).
Walitalikiana mwaka 1987, lakini baadaye aliondoa tuhuma za udhalilishaji dhidi ya Puzder wakati wa makubaliano kuhusu nani angewatunza watoto.
WaandamanajiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatetezi wa kuongezwa kwa kiwango cha chini cha ajira waliandamana makao makuu ya Hardee mapema wiki hii
Mawaziri

Mada zinazohusiana

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...