» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: TUFANYEJE?

USHINDI HATIMAYE- TUFANYEJE?
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
MAFUNGU: Ufun 17:3-5;1korinth 11:2;Ufun 12:1-17;Isaya 51:16;Ezek 4:6;Yerem 6:2
“Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu..” (Ufununo 12:17)
Katika biblia lugha ya kiunabii Joka humaanisha Ibirisi(Shetani), mwanamke anawakilisha Kanisa. Biblia ikisema mwanamke kahaba maana yake ni kanisa linafundisha kinyume na Mwenyezi Mungu. Na biblia ikisema Mwanamke safi katika unabii anawakilisha kanisa la Mungu.Ushuhuda wa Yesu ni Maandiko Matakatifu(Biblia).
Ni bayana mbinu atumiayo shetani ni mafundisho potofu au maandiko nusunusu au kubadili Amri za Mungu na kuwafanya wanadamu wasizishike amri za Mungu kwani uadui wake ni dhidi ya kanisa lishikalo amri za Mungu na ushuhuda wa Imani ya Yesu. Vita kati ya Mungu na Shetani ni juu ya SHERIA ZA MUNGU, shetani anakataa kumtii Mungu akidai na yeye kuwa ni sawa na Mungu.Si kila ahubiriye yuko upande wa Mungu,hata shetani joka wa zamani hutumia vifungu vya biblia kutetea hoja zake zisizo na mashiko na siyo kuiacha Biblia nzima ijipambanue kwa uhalisia wa hoja.
Na katika hili ieleweka kwamba kipimo cha Imani yako ni Biblia takatifu ambayo ina muelezea Mungu kama MFALME wa Mbingu na Nchi na Si mwanademokrasia au Mungu wa wengi wape.Maana Yeye mwenyewe alisema “Usiwe na miungu mingine ila Mimi. Mawazo ya wataalamu, na tafsiri potofu za Biblia wanazoeleza watu wa sayansi, na mashauri hayana nafasi kwani Mungu atakuwa na watu wenye kushika Biblia na mafundisho yake peke yake, kuwa ndiyo kanuni ya maisha.
Kanisa la Mungu ni lile ambalo kuinuka kwake, kunakuja baada ya miaka 1260 yaani baada ya mwaka 1798 na kushambuliwa na Shetani (Uf. 12:6, 17). Lina imani ya Yesu na linatii amri za Mungu zisizobadilika (Kut. 20: 1- 17) na lina ushuhuda wa Yesu ambao ni Roho ya Unabii (Uf. 19:10).
Mungu anapotuma maonyo, hutazamia kuwa kila mtu atatega sikio na kuyajali, lakini makundi mengi hawaelewi ukweli huu muhimu. Wale wanaojitahidi kushika amri za Mungu, watapingwa na kudhihakiwa. Ili kusudi waweze kusimama na kushinda, ni lazima wafahamu mapenzi ya Mungu jinsi yalivyofunuliwa katika Biblia.LIFATE KANISA LA MUNGU ALIYE HAI, HAJAKUFICHA BALI AMEKUONESHA. AMEN

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...