» » USHINDI HATIMAYE - SOMO: JE WEWE UTAWEZA?

USHINDI HATIMAYE - JE WEWE UTAWEZA?
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church

MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
WADHAMINI: Chama cha Wajasiriamali na Wanataalum(ATAPE) wakishirikiana na Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini.
MAFUNGU: Mathayo 5:38-41;1 Samwel 24:1-5;1 Samwel 24:5-8;Zaburi 119:11;Mathy 7:12
"Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana" (Warumi 12:19)
Kuna matatizo mengi katika ukoo,marafiki, ndoa,kazini,majirani ni kwa sababu tumekuwa tukifanyiwa ubaya nasi tunalipiza kisasi. Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya jirani yako,fahamu mabaya hayata ondoka nyumbani kwako. Ikiwa ni sehemu ya kazi,mabaya hayataondoka hapo kazini maana chochote ampandacho mtu ndicho atakachovuna.
Kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo,tusishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.Mungu amekupatia jirani mkorofi,bosi mkorofi ili aitengeneze tabia yako uwe mkristo wa kweli. Ukiamua kulipa kisasi elewa hiyo vita Mungu atanyamaza hata kuwa upande wako kwani gadhabu ya Mungu iko juu yao walipao kisasi. Maana "imeandikwa kisasi ni juu yangu MIMI; Mimi nitalipa, anena Bwana".
Ukihitaji kushinda dhambi ya chuki,mfanye MUNGU kuwa wa kwanza kama Daudi alivyojinyenyekeza kwa Bwana japo alikuwa na vita ngumu;alikubali kuliweka neno la Mungu moyoni mwake ili asimtende dhambi Mungu. Kipimo unachopima ndicho utakachopimiwa,adui akiwa na njaa mlishe.Mkaribishe Yesu awe Mwongozi Wako.
Mtu akikufanyia ubaya, usione kuwa anakufanyia wewe, ona kama vile Mungu aonavyo kuwa, ubaya huo anafanyiwa Kristo aliye ndani yako.Mtu akikutukana, akikusemea mabaya, akikupiga, fahamu kuwa si wewe anayekufanyia hayo, bali Kristo aliye ndani yako.
Hata kama una chuki,roho ya adui Bwana ataiondoa ukijisalimisha kwake.Vaa Ujasiri mpigie adui yako mwambie nimeamua kumshinda adui kwa kuondoa chuki dhidi yako. Kubali Mungu akutengeneze sasa nawe utakuwa MSHINDI.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...