USHINDI HATIMAYE- VITA MAISHANI
Mhubiri: Mchungaji David Mbaga
Mhali: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza katika mahubiri yaliyo dhaminiwa na chama cha wanataaluma na wajasiriamali(ATAPE)
Mhali: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza katika mahubiri yaliyo dhaminiwa na chama cha wanataaluma na wajasiriamali(ATAPE)
Mafungu: 1 samwel 16:1-23; 1samwel 17-1-16;Ebrania 11:4-32
“ Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda”.(Warumi 8:37)
Nani ambaye hajawahi kupambana? mkristo anayo vita anayopaswa kupigana katika maisha haya. Ingawa vita si jambo linawafurahisha watu wengi.Mkristo apaswa kupigana vita ya kiroho(IMANI) ambayo ni tofauti na vita ya kimawazo, vita ya kijamii inayo husisha ubaguzi wa rangi,kabila na matabaka mbalimbali.
Wapo watu walipigana vita ambao biblia takatifu inawataja kama Enocko ambaye alitembea na Mungu wakati wote,Nuhu ambaye alipata neema machoni pa Bwana, Abili ambaye alikuwa mshindi japo ilimgharimu mauti lakini aliisikiliza sauti ya Mungu, bila kumsahau Daudi ambaye alipata ushindi kwa nguvu za MUNGU –BWANA WA MAJESHI ASIYE SHINDWA.
DAUDI akasema “asizimie moyo mtu yeyote kwa ajili ya huyu, mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na mfilisti huyu.” Mpendwa usizimie moyo kwa ajili ya jambo hilo (Ukosefu wa ajira, madeni,ugonjwa, fitina, umasikini nk) maana katika yote tunaye atushindiaye, Kristo atayamulika mapito yako na kukushika kwa mkono wake wa kuume pale tu utakapoamua kumwamini kwa moyo wako wote,SIKILIZA SAUTI YA MUNGU IKIKUITA.
Waweza kufanya mambo makubwa ya kumpendeza BWANA haijalishi u mdogo wa umri, elimu, umbo dogo,KUMBUKA KULE BWANA ALIKO KUTOA kwani katika BWANA KUNA USHINDI.KUWA USHUHUDA KWA WATU.
Usijadiliane na adui. Wana wa Israeli walitakiwa kujipanga kuvamia, kwa mfano wangeamua watu sita wamvamie Goliathi na wengine wavamie jeshi la wafilisti wangemaliza kelele zote za Goliathi. Kitendo cha kujadiliana na Goliathi kilimpa Goliathi nafasi ya kuingiza hofu mioyoni mwao.
Katika kila jambo, hata kama dunia nzima watasema hili haliwezekani wewe soma LUKA 1:37. “hakuna la kumshinda Mungu”.
UKIBARIKIWA SEMA !AMEN
UKIBARIKIWA SEMA !AMEN
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment