» » KESHA LA ASUBUHIJUMATATU-FEBRUARI 13, 2017

KESHA LA ASUBUHI
JUMATATU-FEBRUARI 13, 2017

KUKARIBISHA WAGENI

Once Saved, Always Saved?
"Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua." WAEBRANIA 13:2.
▶Mungu alimpa Ibrahimu heshima kubwa. Malaika wa mbinguni walitembea na kuzungumza naye kama rafiki azungumzavyo na rafiki. Wakati hukumu ilipokuwa ishushwe kwa Sodoma, hakufichwa ukweli juu ya hili na akawa mpatanishi kwa ajili ya wenye dhambi na Mungu. Vilevile, kuhojiana kwake na malaika kunaonesha mfano mzuri wa ukarimu.
▶Kwenye taarifa za kitabu cha Mwanzo huyu mzee wa imani kwenye joto kali la majira ya kiangazi akiwa amepumzika kwenye lango la hema lake chini ya kivuli cha mialoni ya Mamre. Mara wasafiri watatu wakawa wakipita karibu. Hawakuonesha namna yoyote ya kutaka kukaribishwa, hawakutafuta namna yoyote ya kupata fadhila; lakini Ibrahimu hakuruhusu waendelee katika njia yao wakiwa hawajaburudishwa.
▶Yeye alikuwa mtu wa umri mkubwa, mtu wa heshima na utajiri, ambaye aliheshimika sana na aliyezoea kuamuru; licha ya hayo, alipowaona hawa wageni “alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi.” Huku akinena kumwelekea kiongozi wao alisema: “Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako” {MWANZO- 18:2, 3}.
▶ Kwa mikono yake mwenyewe alileta maji ili wapate kuosha vumbi miguuni pao waliyoipata safarini. Yeye mwenyewe aliwachagulia chakula; huku wakiwa wamepumzika kwenye kivuli, Sara mkewe aliandaa kwa ajili ya kuwaburudisha na Ibrahimu alisimama kwa heshima kando yao wakati wakishiriki ukarimu wake. Wema huu aliuonesha kwao kama wapiti njia tu, wageni wanaopita, ambao ingewezekana wasije tena katika njia yake. Lakini, baada ya kufurahia chakula, wageni wake walidhihirika. Alikuwa amehudumia sio malaika wa mbinguni tu, bali Kamanda wao aliyetukuka, Muumbaji wake, Mkombozi na Mfalme. Tena kwa Ibrahimu, mashauri ya mbinguni yakafunguliwa na akaitwa “rafiki wa Mungu.”….
▶Sisi hatujanyimwa fadhila ambayo Ibrahimu na Lutu walipewa. Kwa kuonesha ukarimu kwa watoto wa Mungu, sisi pia, tunaweza kupokea malaika kwenye makazi yetu. Hata wakati wetu huu, malaika huingia nyumbani mwa watu na kukirimiwa wakiwa katika mwonekano wa kibinadamu. Na Wakristo wanaoishi katika nuru ya uso wa Mungu daima husindikizwa na malaika wasioonekana na viumbe hawa watakatifu huacha nyuma yao baraka kwenye nyumba zetu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...