» » Usajili wa TIN wafikia kikomo

Usajili wa TIN wafikia kikomo

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haitaongeza siku za kufanya uhakiki wa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) hapa jijini baada ya muda kumalizika leo, hivyo wote watakaokuwa hawajahakikiwa watafutiwa namba zao na watatakiwa kuomba upya.

Kwa mara ya kwanza TRA imepanga kufanya uhakiki wa TIN kwa siku 60 kati ya Agosti na Oktoba lakini baada ya kujitokeza watu wengi tarehe ya mwisho iliongezwa hadi Novemba na mara ya tatu ilisogezwa hadi Januari 31. Lengo la uhakiki huo ni kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo.

Kayombo alisema kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanahitaji kuhakikiwa namba, mamlaka iliamua kusogeza mbele muda wa kutoa huduma hiyo pamoja na kufungua vituo vya kutoa huduma ambako watumishi walifanya kazi hiyo hadi Jumamosi na Jumapili kuwapa nafasi wafanyakazi.

Alisema madhara kwa watakaofutiwa TIN ni makubwa kwani wafanyabiashara na madereva wa magari leseni zao zitakuwa batili na watachukuliwa hatua kwa kosa la kufanya biashara bila kuwa na namba ya utambulisho.

“Wale wote ambao watakuwa hawajahakikiwa watafutiwa namba zao za TIN, itawalazimu kuomba upya ingawa kuomba kwao upya hakutafuta madeni yao ya nyuma,” alisisitiza Kayombo.

Mmoja wa watu waliokwenda kuhakiki namba zao kituo cha Mwenge, Abdul Namwelesi alikosoa utaratibu huo akipendekeza uhakiki ungekuwa endelevu badala ya kuweka muda maalumu kutokana na ugumu wa watu wote kuhakikiwa kwa wakati mmoja.

Alisema kutokana na ratiba ya maisha hususani kwa wakazi wa Dar kuwa za kukimbizana, TRA wangeweka utaratibu maalumu kila dereva anapokwenda kuhuisha leseni yake ahakikiwe taarifa zake  na kila mfanyabiashara anapokwenda kulipa kodi hapohapo ahakikiwe taarifa zake.

Zulekha Kambi aliyekutwa kwenye kituo cha Uwanja wa Taifa alijilaumu kutokana na kutotumia muda mrefu uliokuwa umetolewa badala yake akasubiri hadi siku za mwisho zenye msongamano mkubwa.

“Najuta. Wee acha tu. Nilikuwa likizo nyumbani mwezi mzima. Jana ndiyo nimekumbuka kesho mwisho. Nimekuja na nimekuta umati kama huu. Hapa nilipo hata fomu sijui nitaipata saa ngapi,” alisikitika.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...