» » Hali mbaya uwanja wa Sheikh Amri

Hali mbaya uwanja wa Sheikh Amri

Arusha. Hali mbaya ya vyumba vya kubadilisha nguo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri, Arusha unahatarisha afya za wachezaji wanaoutumia.

 Hali hiyo, ambayo imesababisha hata kipindi cha mapumziko kushindwa kukaa vyumbani imekuwa kero kwa watumiaji.

Uwanja huo unaotumiwa na timu nne zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara, umekuwa na mazingira mabovu kiasi cha wachezaji kulazimika kukaa uwanjani wakati wa mapumziko kutokana na hali mbaya ya vyumbani.

Vyoo vilivyopo kwenye vyumba vya wachezaji vimekuwa  vichafu na umeme umekuwa si wa uhakika pamoja na ubovu wa sehemu ya kuchezea kuwa kipara kutokana na ukosefu wa majani lakini pia umetawaliwa na mashimo katika eneo la kuchezea.

Gazeti hili lilishudia hali hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa mechi iliyowakutanisha watoto wa nyumbani Pepsi FC na Arusha FC, wachezaji walishindwa kuingia vyumbani kubadili nguo wakati wa mapumziko na kuamua kukaa uwanjani.

Mechi hiyo iliyomalizika kwa timu ya Pepsi kushinda kwa bao 1-0 dakika ya 40 lililoingizwa kimiani na Eliriki Herman walilazimika kubadili nguo hadharani huku wakishuhudiwa na mashabiki wao.

Akizungumzia hali ya uwanja huo wachezaji hao wa walisema walishindwa kupumzika vyumbani kutokana na hewa nzito iliyokuwa ndani ya vyumba hivyo, ambavyo pia vilikuwa giza kutokana na umeme kukatika.

“Hewa ni nzito mno humo ndani na inaonekana hawajafanya usafi maana hata vyoo ni vichafu halafu hakuna maji tunajisaidiaje huko zaidi ya yote ni giza balaa maana hivyo vyumba havina madirisha bali tunategemea umeme hata kuchukua tahadhari, sasa umeme leo haupo, fikiria kama wewe ni binadamu tunakaaje humo.”

Meneja wa uwanja huo, Jackson Joorwa alisema vyumba hivyo vimekuwa giza kutokana na kukatika kwa umeme na uwanja hauna jenereta. “Suala la kiwanja cha kuchezea uongozi wa juu unashughulikia na ukarabati unaanza mara moja, lakini suala la umeme liko nje ya uwezo wangu maana unaona mwenyewe kuwa mji mzima hauna umeme. Na Jenereta pia tatizo, nifanyeje?”

Msimamizi wa mechi hiyo (kamisaa) Beda Lyimo alisema ni kosa wachezaji kugoma kuingia vyumbani na ameshaandikia taarifa.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...